Jinsi ya Kutunza Kitovu cha Mtoto

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kovu kwenye Kitovu ni alama kuwa wakati fulani katika maisha yako ulikuwa unamtegemea mtu mwingine. Wakati uko tumboni kwa mama yako kitovu kina mishipa ya damu ambayo kazi yake kubwa ni kutoa chakula kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa uchafu kwa mtoto kwenda kwa mama ili utolewe nje.

Mara baada ya kujifungua kitovu kinakatwa na kubanwa ili kuzuia damu kuvuja. Sasa mwanao atakuwa na kipande cha kitovu chenye urefu wa inchi moja ama inchi moja na nusu. Kitovu kisipotunzwa kwa uangalifu kinaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya bakteria kwa mtoto.

Mambo ya kufanya

Zingatia usafi

Zamani madaktari walikuwa wanashauri kusafisha kitavu kwa kutumia spirit. Lakini sasa hivi unashauriwa kuacha kitovu kikauke chenyewe bila hata kukigusa. Matumizi ya spirit hufanya kitovu kichelewe kupona.

Acha pakauke

Ni vizuri kuacha kitovu kipigwe na hewa mara nyingi kadri inavyowezekana. Hii inasaidia kitovu kukauka kwa haraka. Iwapo unatumia nepi au pampers unaweza kuzigunja sehemu kitovu ikabaki wazi.

Usimuogeshe mwili mzima

Unaweza kumfuta mtoto wako kwa kutumia kitambaa safi sana maji. Kulowanisha kitovu kunaweza kusababisha kuchelewa kupona.

Acha kipone chenyewe

Usijaribu kuondoa kitovu, acha kidondoke chenyewe.

Je kitovu kinadondoka baada ya muda gani

Kwa kawaida kitovu kinadondoka baada ya wiki moja mpaka wiki mbili. Iwapo kitovu cha mtoto hakijadondoka baada ya huo muda unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa afya.

Dalili za maambukizi kwenye kitovu

Wakati mwingine mtoto anaweza kupata maambukizi ya bakteria kwenye kitovu

Zifuatazo ni dalili za maambukizi hayo:-

▫️Ngozi inayozunguka kitovu kuwa nyekundu

▫️Kitovu kuvimba

▫️Kuvuja damu kwenye kitovu

▫️Kutoa usaha kwenye kitovu/ au uchafu unatoa harufu mbaya

▫️Mtoto kupata maumivu.

Mara tu unapoona dalili yoyote katika ya hizo, nenda hospitali mara moja. Utaandikiwa dawa za kutumia ili kupunguza bakteria kuingia kwenye damu.

Uvimbe kwenye kitovu

Wakati mwingine kitovu hukatika na kuacha uvimbe kama kinyama kwenye shina la kitovu. Tatizo hili hutibiwa kwa dawa ya kuunguza. Dawa hii hutolewa kwa ushauri wa daktari.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment