Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ni rahisi kuamini kuwa ndoto yako ITAFANIKIWA na MALENGO yako yatatimia pale ambapo kuna DALILI nyingi zinazotia MOYO.
Hata hivyo IMANI ya kweli huonekana pale ambapo kila kinachotokea kinaonyesha uwezekano wa KUTOKUFANIKIWA.
Mara nyingi sana KINACHOUA ndoto na MATUMAINI ya watu wengi ni pale WANAPOANGALIA yale YANAYOTOKEA na kuwajengea HOFU ya ndani inayowaonyesha kuwa HAWATAFANIKIWA kabisa.
Leo asubuhi nilikuwa nasoma Biblia nikakutana na mahali ambapo Yesu alikuwa anatembea juu ya maji na alimuita Petro ashuke kwenye boti ili atembee juu ya maji na amfuate alipo.

Kwa hatua kadhaa Petro aliweza kutembea ila imeandikwa “Alipoona UPEPO MKALI, alipata HOFU na AKAANZA KUZAMA”.
Kitu kikubwa nilichojifunza ni kuwa, kilichokuwa KINAMZAMISHA Petro sio upepo mkali ila ni ile HOFU aliyopata baada ya kuona upepo mkali.
Kwani katika upepo huo mkali, Yesu aliweza kuendelea kutembea na HAKUZAMA.
Kinachozamisha NDOTO, MAONO na MIPANGO ya watu wengi sio MAGUMU yanayotokea.
Sio UPINZANI unaokutana nao.
Sio RASILIMALI unazokosa.
KINACHOKUZAMISHA ni HOFU ambayo inaua IMANI yako juu ya KESHO YAKO.
Kama hautaki KUZAMA kwenye maisha yako anza siku kwa kusema – “SITARUHUSU HOFU ya aina yoyote ile IZAMISHE NDOTO ZANGU…

.
…Naamua kuwa na IMANI ya KUFANIKIWA bila KUJALI DHORUBA zinazonizunguka LEO”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.