Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

John D. Rockefeller aliwahi kusema… “The secret of success is to do the common things uncommonly well”
(Siri ya mafanikio ni kufanya kitu cha kawaida katika ubora wa juu na Namna Isiyo ya kawaida).
Watu wengi sana huwa wanasubiri kufanikiwa pale watakapopata Fursa kubwa zaidi ya walizonazo sasa hivi…
…ama watakapokutana na watu wakubwa zaidi kimamlaka ama kiuwezo ndipo wafanye kwa ubora na wapate matokeo Makubwa.
Kwa mujibu wa bilionea wa kwanza kuwahi kutokea marekani, John D Rockefeller anasema ukisubiria namna hiyo utachelewa sana kufanikiwa.
Wewe unachotakiwa kufanya ni kilekile kinachoonekana cha kawaida wewe uamue kukifanya kwa namna isiyo ya kawaida hadi kila mtu ashangae.
(Take common thing and make it special).
Kama unauza juice ifanye kwa namna ya kipekee, kama unauza mitumba tafuta namna ya kujitofautisha.
Ukipewa nafasi usiidharau tafuta namna ya kufanya isivyo kawaida n.k
Inawezekana nafasi uliyonayo inadahraulika, tafuta namna ya kufanya kwa kiwango ambacho sio cha kawaida hadi watu washangae.
Inawezekana biashara unayofanya inaonekana haina nguvu, fanya kwa namna ambayo kila mtu atashangaa jinsi utakavyofanikiwa n.k
Hii ndio maana unaweza kukuta mtu anapewa cheo ambacho zamani kilikuwa kinadharaulika lakini yeye anafanya vitu hadi watu wanashangaa.
Au unakuta anafanya biashara ya kawaida na anafanikiwa kwa kiwango ambacho kila mtu anashangaa.
USISUBIRI upande zaidi au uwe na vingi ili UFANYE kwa ubora zaidi, anza leo.
Je, unapanga kufanya nini leo ili kujitofautisha na ulivyokuwa unafanya kila siku?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.