Maisha Jessica Cox……..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jessica cox ni mwanamke mmarekani aliyezaliwa mnano mwaka 1983 bila mikono lakini ndiye mwanamke pekee wa kwanza asiye na mikono pekee duniani kupewa leseni ya kurusha ndege, mwanamke rubani asiye na mikono hivyo anaongoza ndege kwa kutumia miguu yake!

.

Na huu ndio upekee wake mkubwa kwa marubani wote duniani ukiangalia kwa hali ya kawaida hana viungo ambavyo ni mikono inayotumika kuongozea ndege lakini kwake kutumia miguu ndicho kimekua kitu chake cha pekee sana na kujitofautisha sana rubani yoyote Duniani na ndicho kinaishangaza dunia kutoka kwake!

.

Katika kitabu chake cha “Disarm your Limits” moja ya msemo wake anasema katika maisha huitaji kuwa na mikono ili uwainue watu kutoka chini ila unahitaji moyo wa Upendo wa kudhati kuwatia moyo na kuwaonesha wanaweza kufanya Makubwa haijalishi walivyo haikua rahisi kwangu kuthubutu kufanya ninachofanya,haikua rahisi nikijiona nilivyo na maamuzi ya kujifunza urubani!

.Anasema haijalishi ulivyo na watu wanakuonaje unahitaji mambo muhimu sana kama.

.

Kujiamini mwenyewe hata kama wengine hawakuamini, haikua rahisi watu kuamini kama ntaweza kuongoza ndege bila mikono sasa naongoza, unahitaji uvumilivu mkubwa, unahitaji kujaribu Mara mia Mara elfu mpaka uweze, unahitaji kushindwa Mara nyingi ili ushinde, unahitaji kushinda roho ya uoga na anasema vikwazo vingi vinavyotuzuia ni kwa sababu ya mtazamo wetu hua tunavitengeneza wenyewe kiuhalisia havipo!

.Amini wewe ni mashindi hata kama hakuna anayeamini wewe ni mshindi kwa sababu ya muonekano wako wa nje lakini jiamini na jikubali mwenyewe jinsi ulivyo ushindi uko ndani yako!.

.

Jifunze jambo kutoka kwa Jessica cox rubani asiye na mikono!

.

Kitu ambacho kinaonekana ni udhaifu wako hicho kinaweza kuwa fursa ya kuishangaza dunia na ndicho kinaweza beba tofauti yako na THAMANI yako!

USIKATE TAMAA JINSI ULIVYO UNAWEZA UNA UKUU NDANI YAKO!

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment