“Wao wameshasema,je wewe unasemaje?”.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.Kuna watu kila siku wanasema hawawezi kufanya mambo makubwa na kusonga mbele kwa sababu fulani aliwaambia wao si kitu.

.

Bosi aliwaambia hawawezi chochote,mzazi au rafiki amewaambia hawatafika mbali,kuna kiongozi amewatamkia hawana maana Je,wewe umejiambiaje?

.

Mume wako kakuambia wewe si kitu, hauwezi chochote na hautafika mbali.

.

Usisahau dunia yetu imejaa watu WALIOKATA TAMAA na ambao ni mahodari wa KUVUNJA wengine MIOYO.Watu hawa hata leo utakutana nao.Nia yao kubwa ni “KUUA MBEGU YA UKUU ILIYOKO NDANI YAKO”-Usiwaruhusu.

.

Ukiruhusu maneno haya yaingie moyoni mwako utajikuta kila unapomwangalia mtu mwingine aliyefanya jambo fulani utaanza kujiambia “Huyu jamaa ni very special”. Utaanza kuamini kuwa wewe hauko katika orodha ya watu wa kipekee wanaoweza kufanya mambo makubwa kwenye maisha.

…..Ukiendelea hivi utaondoka duniani bila kuishi ndoto yako na kutimiza malengo yako.

.

Badala ya kila siku kuendelea kulalamika jinsi wengine walivyosema hauwezi,hautafika mbali,wewe si kitu n.k anza kujiuliza-Wewe mwenyewe umejiambiaje?Umekubaliana nao?

.

Kumbuka wengi ambao watakuwa wanakuambia maneno haya ukiwaangali unakuta wenyewe hawajafanya jambo kubwa lolote, ni ule wivu wa kuogopa kuwa utafanya kitu na kung’aa ndio unaowasumbua.

.

Leo wewe unajiambiaje?Mimi nilichagua kujiambia “Bila kujali kitakachosemwa,nimechagua kuishi ndoto yangu na kutimiza malengo yangu,am going to the top”.

.

USIRUHUSU WALE AMBAO HAUJUI UWEZO ULIO NDANI YAKO WAKUWEKEE MIPAKA YA KILE UNACHOWEZA KUFANYA.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment