Unapochelewa…..

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

HISIA ZA KUCHELEWA zimesababisha watu wengi sana wafanye maamuzi waliyoyajutia maishani mwao.

Kuna watu walipata presha na kuona kuwa wamechelewa kupata mwenzi.

Matokeo yake walijiingiza kwenye mahusiano ambayo yalikuwa ndio chanzo cha mateso yao…

…kupoteza mwelekeo na kuwakosesha furaha siku zote.

Kuna wengine wamejikuta wameingia kwenye matatizo ya kifedha…

Kesi na kugombana na watu kwa sababu…

…walipohisi wamechelewa walijiingiza kwenye njia za mkato za kutafuta mafanikio.

Hisia za kuchelewa zimewafanya watu wapoteze utu wao.

Wavunje miiko yao na hata wengine waingie kwenye utumwa wa maisha…

…ili tu wapate NAFASI FULANI.

Usisahau kuwa, Mungu huwa hachelewi wala hawahi…

…huwa anafanya kwa majira na wakati wake.

Ukianza kujitengenezea njia yako kwa sababu unaona Mungu anachelewa…

…atakuacha peke yako na utajikuta umeelekea kusiko sahihi.

Endelea kumtumaini Mungu na kufanya yaliyo sahihi bila kuacha…

…usiruhusu presha ya watu kukuonesha kuwa umechelewa ikupelekee kufanya maamuzi yasiyo sahihi…

…ambayo yatakuwa na MAJUTO baadaye.

Kesho yako ni Njema.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment