Israel inajiandaa ‘kuchukua udhibiti’ wa Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mpango huo unakabiliwa na upinzani mkali ndani ya Israeli – ikiwa ni pamoja na maafisa wa kijeshi na familia za mateka.

Wengine watano wafa kwa utapiamlo Gaza katika saa 24 zilizopita

d
Maelezo ya picha,Hamza Mishmish, 25, huko Gaza anaonyesha dalili za utapiamlo katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat huku kukiwa na njaa. Picha hii ilipigwa Julai 27.

Katika saa 24 zilizopita, watu watano wamekufa kutokana na utapiamlo, kulingana na taarifa ya hivi punde kutoka kwa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Hiyo inaifanya jumla ya vifo vya utapiamlo kufikia 222, inasema wizara hiyo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu lilisema siku ya Ijumaa kwamba kiasi cha misaada inayoingia Gaza kinaendelea kuwa “chini ya kiwango kinachohitajika kukidhi mahitaji makubwa ya watu.”

Israel imekanusha kuwa kuna njaa huko Gaza na kuyashutumu mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutochukua misaada katika mipaka na kuipeleka Gaza.

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu linasema linaendelea kuona vikwazo na ucheleweshaji wakati linajaribu kukusanya misaada kutoka maeneo ya mpaka yanayodhibitiwa na Israel.

Wakati huo huo Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema watu 69 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hiyo inaifanya idadi ya Wapalestina waliouawa tangu kuanza kwa vita kufikia 61,499, huku zaidi ya watu 150,000 wakijeruhiwa, kulingana na wizara hiyo.

Israel inajiandaa ‘kuchukua udhibiti’ wa Gaza

df

Jeshi la Israel linajiandaa “kuchukua udhibiti” wa mji wa Gaza, uamuzi huo ulitolewa wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri la usalama la Israel wiki iliyopita, lakini umekabiliwa na upinzani wa ndani na kimataifa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa mpango huo ndio “njia bora” ya kumaliza vita, lakini washirika kadhaa wa Israel wamelaani wazo hilo, huku Umoja wa Mataifa ukionya kuwa litasababisha “watu wengi zaidi kukimbia makazi yao na “mauaji zaidi.”

Hamas inapinga vikalihatua hiyo.

Mpango huo pia unakabiliwa na upinzani mkali ndani ya Israeli – ikiwa ni pamoja na maafisa wa kijeshi na familia za mateka.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinasema vinajiandaa kuudhibiti mji wa Gaza huku wakitoa misaada ya kibinadamu kwa “raia walio nje ya maeneo ya mapigano.”

Makumi ya wanajeshi wakamatwa Mali kwa madai ya njama ya mapinduzi

d
Maelezo ya picha,Kiongozi wa kijeshi Jenerali Asimi Goïta alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mawili mwaka 2020 na 2021.

Makumi ya wanajeshi wamekamatwa nchini Mali wakituhumiwa kupanga njama ya kuwapindua viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, taarifa zinaeleza.

Wimbi la kukamatwa kwa watu hao, ambalo limeripotiwa kuendelea usiku kucha na linatarajiwa kuendelea, linaonyesha mvutano ulioongezeka ndani ya serikali ya kijeshi, huku ripoti zikisema kuwa uasi wa kijihadi kaskazini unazidi kushika kasi.

Serikali haijatoa maoni yoyote kuhusu kukamatwa kwa watu hao.

Ripoti za awali zilionyesha kuwa Jenerali Abass Dembele, gavana wa zamani wa eneo la Mopti na Jenerali Nema Sagara, mmoja wa wanawake wachache katika ngazi za juu zaidi za jeshi la Mali, walikuwa miongoni mwa waliokamatwa.

Hata hivyo, chanzo kilicho karibu na Jenerali Dembele kiliambia BBC hakuna hata mmoja wao aliyekamatwa kati ya wawili hao.

Shirika la habari la AFP liliripoti kuwa wanajeshi waliozuiliwa wanadaiwa kupanga kupindua serikali, likitaja vyanzo vingi ndani ya jeshi na baraza la mpito linaloungwa mkono na jeshi.

“Wote ni wanajeshi. Lengo lao lilikuwa kupindua jeshi,” lilimnukuu mbunge ambaye hakutajwa jina katika Baraza la Kitaifa la Mpito.

Alisema “waliokamatwa 50,” huku chanzo kingine kikisema watu wasiopungua 20 ndio waliokamatwa, AFP inaripoti.

Kukamatwa kwa watu hao kumeripotiwa kuendelea kwa siku kadhaa.

Hayo yanakuja huku kukiwa na mvutano wa kisiasa uliochochewa na msako wa serikali ya kijeshi dhidi ya Mawaziri Wakuu wa zamani Moussa Mara na Choguel Maiga kwa tuhuma za kuharibu sifa ya serikali na ubadhirifu.

Mara, mkosoaji wa serikali ya kijeshi, amekuwa kizuizini tangu tarehe 1 Agosti, huku Maiga akikabiliwa na vikwazo vya mahakama.

Mwezi Mei, serikali ya kijeshi ilivifuta vyama vyote vya kisiasa kufuatia maandamano ya nadra dhidi ya serikali, ambayo Mara aliyataja kuwa pigo kubwa kwa juhudi za maridhiano zilizoanzishwa na viongozi wa kijeshi mwaka jana.

Kiongozi wa serikali ya kijeshi Jenerali Asimi Goïta, ambaye alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mawili mwaka 2020 na 2021, aliahidi uchaguzi mwaka jana, lakini haya hayajawahi kufanyika.

Mnamo Julai, kipindi cha mpito kiliongezwa kwa miaka mitano, na kumruhusu kuendelea kuongoza nchi hadi 2030.

Mali imekuwa ikipambana na waasi wa Kiislamu tangu mwaka 2012 – moja ya sababu zilizotolewa za kuwepo serikali ya jeshi lakini mashambulizi ya makundi ya kijihadi yameendelea na kuongezeka.

Pamoja na majirani zake Niger na Burkina Faso, imeomba usaidizi wa Urusi ili kudhibiti mashambulizi ya wanajihadi katika eneo hilo baada ya kuvunja uhusiano na Ufaransa.

Hasira zaibuka baada ya mtoto kukeketwa na kufariki

fv
Maelezo ya picha,Jaribio la kuruhusu ukeketaji nchini Gambia lilizuiwa na kampeni ya wanawake mwaka jana

Kifo cha mtoto wa kike wa mwezi mmoja mwathiriwa wa ukeketaji nchini Gambia kimeibua hasira kubwa.

Mtoto huyo alikimbizwa hospitali katika mji mkuu, Banjul, baada ya kutokwa na damu nyingi, lakini alitangazwa kuwa amefariki alipofika, wamesema polisi.

Ingawa uchunguzi wa maiti bado unafanywa ili kubaini sababu ya kifo chake, watu wengi wamehusisha na ukeketaji, au tohara ya wanawake, utamaduni ulioharamishwa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wanawake wawili wamekamatwa kwa madai ya kuhusika katika kifo cha mtoto huyo, polisi wamesema.

Mbunge wa Jimbo la Kombo Kaskazini lilikotokea tukio hilo alisisitiza kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu vinavyowakosesha afya, utu na maisha.

Ukeketaji ni kukata au kuondoa kwa makusudi sehemu ya siri ya nje ya mwanamke.

Sababu zinazotajwa mara kwa mara za kuitekeleza ni kukubalika katika jamii, imani za kidini, imani potofu kuhusu usafi, njia ya kuhifadhi ubikira wa msichana au mwanamke, kumfanya “aolewe”, na kuimarisha furaha ya mwanaume.

Gambia ni miongoni mwa nchi 10 zilizo na viwango vya juu vya ukeketaji, ambapo asilimia 73 ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa utaratibu huo, huku wengi wakifanyiwa hivyo kabla ya kufikia umri wa miaka sita.

Ukeketaji umeharamishwa nchini Gambia tangu 2015, na kuna faini na vifungo vya hadi miaka mitatu jela kwa wahalifu, na kifungo cha maisha ikiwa msichana atakufa kama matokeo ya ukeketaji.

Ukeketaji umepigwa marufuku katika nchi zaidi ya 70 duniani kote lakini unaendelea kutekelezwa hasa katika nchi za Afrika zenye Waislamu wengi, kama vile Gambia.

Urusi inasema iliendelea na utengenezaji wa makombora ya nyuklia wakati wa zuio

fc
Maelezo ya picha,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Ryabkov.

Urusi iliendelea na uundaji wa mifumo ya makombora ya masafa ya kati na mafupi ya nyuklia wakati wa zuio na sasa ina safu kubwa ya silaha kama hizo, vyombo vya habari vya Urusi viliripoti mwishoni mwa Jumapili vikimnukuu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Ryabkov.

“Wakati zuio lilipotangazwa, tuliweka wazi kuwa linahusu tu kuzisafirisha, na halikutaja kuzuia shughuli za utafiti na utengenezaji,” shirika la habari la RIA lilimnukuu Ryabkov.

“Kwa hivyo wakati huu ulitumika kukuza mifumo inayofaa na kujenga safu kubwa ya silaha,” RIA ilimnukuu Ryabkov.

Mapema mwezi huu, Urusi ilisema inaondoa kile ilichokiita ‘kusitisha’ usafirishaji wa makombora ya masafa ya kati ya nyuklia ikisema hilo ni jibu kwa hatua za Marekani na washirika wake.

Katika taarifa Jumatatu iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi alihusisha uamuzi huo na juhudi za Marekani na washirika wake kutengeneza silaha za masafa ya kati na maandalizi ya kupelekwa Ulaya na sehemu nyingine za dunia.

Akitaja haswa mipango ya Marekani ya kupeleka makombora ya Kimbunga na Dark Eagle nchini Ujerumani kuanzia mwaka ujao.

Mkataba wa makombora ya masafa mafupi na wa kati, uliotiwa saini na Umoja wa Kisovyeti na Marekani 1987 ulionekana wakati huo kama ishara ya kupunguza mvutano kati ya mataifa makubwa pinzani. Lakini baada ya muda, ulivunjika wakati uhusiano ulizorota.

Merika ilijiondoa katika mkataba huo 2019 wakati wa urais wa kwanza wa Donald Trump, ikitaja madai ya ukiukaji ambao Urusi ilikanusha.

Korea Kaskazini yaonya kuwa ‘itajibu’ mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani

d
Maelezo ya picha,Kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong-Un katika mkutano na waandishi wa habari Juni 19, 2024.

Korea Kaskazini imekosea mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani kama “uchochezi wa moja kwa moja wa kijeshi” na kuonya kuwa itachukua hatu za kujibu.

Onyo hilo linakuja huku kukiwa na dalili za kupungua kwa mvutano mpakani wa nchi hizo chini ya kiongozi mpya huko Seoul.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini No Kwang Chol amesema jeshi lake lina “dhamira” ya kutetea usalama wa kitaifa dhidi ya mazoezi makubwa ya siku 11 ya Korea Kusini na Marekani, ambayo amesema ni tishio la wazi na hatari.

“Vikosi vya jeshi vitakabiliana na mazoezi ya vita ya Marekani na Kusini kwa hatua kali,” No alisema katika taarifa iliyotolewa kupitia shirika la habari la serikali ya KCNA siku ya Jumatatu.

Korea Kaskazini mara kwa mara inakosoa mazoezi ya kijeshi ya Kusini na Marekani, na kuita mazoezi kadhaa ya hapo awali kuwa ni “mazoezi” ya vita vya nyuklia kwenye peninsula ya Korea, hata kama Pyongyang hufanya mazoezi kwa kutumia silaha nzito na makombora pia.

Korea Kusini na Marekani zilisema wiki iliyopita mazoezi ya kila mwaka yataanza Agosti 18 chini ya mkakati ulioboreshwa dhidi ya tishio la vita vya nyuklia kutoka Korea Kaskazini.

Uhusiano kati ya Korea mbili umetumbukia katika maeneo yenye uhasama zaidi katika miaka ya hivi karibuni, huku Kaskazini ikiendelea kukuza uwezo wa kutumia nyuklia na kuimarisha uhusiano wa kijeshi na Urusi.

Hadi sasa Pyongyang imekataa hadharani kufanya mawasiliano mapya na Lee na Washington kwa ajili mazungumzo, lakini imekuwa ikichukua hatua za chini chini za kupunguza mvutano.

Korea Kusini ilisema Jumamosi kuwa imegundua jeshi la Kaskazini likiondoa vipaza sauti mpakani, siku chache baada ya Kusini kuanza kuondoa vifaa kama hivyo ambavyo vilikuwa vikitumika kwa propaganda.

Korea Kaskazini pia imeonekana kutumia kauli nyepesi zaidi katika ukosoaji juu ya mazoezi ya pamoja ya Marekani na Korea Kusini, alisema afisa katika Wizara ya Muungano ya Seoul, ambayo inasimamia uhusiano kati ya Korea mbili.

Pyongyang “inaonekana kuelezea msimamo wake juu ya mazoezi hayo, badala ya kutoa vitisho vya kijeshi,” msemaji wa wizara Koo Byoungsam alisema katika mkutano Jumatatu.

New Zealand inafikiria kulitambua taifa la Palestina

fc
Maelezo ya picha,Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters

Nchi ya New Zealand inafikiria kulimbuliwa taifa la Palestina, Waziri wa Mambo ya Nje Winston Peters amesema leo siku ya Jumatatu.

Baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Christopher Luxon litafanya uamuzi rasmi mwezi Septemba na kuwasilisha msimamo wa serikali hiyo kwa Umoja wa Mataifa, alisema.

Nchi kadhaa zikiwemo Australia, Uingereza na Canada zimetangaza katika wiki za hivi karibuni kwamba zitalitambua taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa mwezi Septemba.

“Tunakusudia kulipima suala hilo kwa uangalifu na kisha kufanya maamuzi kulingana na kanuni, maadili na maslahi ya kitaifa,” Peters alisema katika taarifa yake.

“New Zealand imekuwa wazi kwa muda kwamba utambuzi wetu wa taifa la Palestina ni suala la lini, sio ikiwa,” Peters aliongeza.

Wito wa kususia bidhaa za Marekani waibuka India kufuatia ushuru wa Trump

fc

Kutoka McDonald’s na Coca-Cola hadi Amazon na Apple, mashirika ya kimataifa ya Marekani yanakabiliwa na wito wa kususiwa nchini India huku wakuu wa biashara na wafuasi wa Waziri Mkuu Narendra Modi wakichochea hisia za kupinga ushuru wa Marekani.

kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, India, taifa lenye watu wengi ulimwenguni, ni soko muhimu kwa bidhaa za Marekani. Ndio soko kubwa zaidi la watumiaji wa WhatsApp ya Meta na Domino ina mikahawa mingi kuliko kampuni nyingine yoyote nchini humo.

Vinywaji kama vile Pepsi na Coca-Cola mara nyingi hutawala rafu za maduka, na watu hupanga foleni wakati bidhaa mpya za Apple zinapozinduliwa au katika mikahawa ya Starbucks.

Ingawa hakuna dalili ya mauzo kupungua, lakini kuna ujumbe unaokuwa kwenye mitandao ya kijamii na nje ya mitandao, kununua bidhaa za ndani na kuacha bidhaa za Marekani baada ya Donald Trump kuweka ushuru wa 50% kwa bidhaa kutoka India.

Ushuru ambao umetikisa uhusiano kati ya New Delhi na Washington.

Wachezaji wa Harambee Stars kuzawadiwa nyumba kila mmoja iwapo watafuzu robo fainali

.
Maelezo ya picha,Rais Ruto alipowatembelea wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya

Rais wa Kenya William Ruto amewaahidi wachezji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars nyumba kila mmoja wao iwapo timu hiyo itafuzu robo fainali na fainali.

Akizungumza baada ya kuitembelea timu hiyo ili kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa kila mchezaji, alioahidi iwapo timu hiyo ingeishinda Morocco amesema ataongeza kiwango cha zawadi hiyo iwapo timu hiyo itafuzu fainali.

‘’Mukifuzu robo fainali hapo unapata shilingi milioni moja yako na nyumba za bei rahisi za vyumba viwili’’, alisema rais Ruto huku wachezaji hao wakifurahishwa na ahadi hiyo.

‘’Tunaelewana …twende polepole kwa masikizano ndio musinichanganye….nahodha unaweka kila kitu katika daftari vizuri’’,? Aliuliza kiongozi huyo wa Kenya.

Hatahivyo rais Ruto alisisitiza kwamba iwapo timu hiyo itailaza timu ya Chipolopolo ya Zambia Jumapili ijayo katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kila mmoja wa wachezaji hao atakabidhiwa shilingi milioni 2.5..

Vilevile aliongezea kwamba iwapo timu hiyo ilioilaza DR Congo , kutoka sare na Angola na kuishinda Morocco itafuzu fainali, atapandisha kiwago cha nyumba atakazowazawadi wachezaji hao kufikia nyumba ya vyumba vitatu.

Kenya inaongoza kundi lao linaloshirikisha Morocco, Zambia, DR congo na Angola katika michuano hiyo ya CHAN inayoandaliwa na nchi tatu za Afrika Mashariki kwa pamoja.

.
Maelezo ya picha,Rais Ruto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee stars

CAF yasimamisha uuzaji wa tiketi za mechi za CHAN katika uwanja wa Kasarani Kenya

RD

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepiga marufuku uuzaji wa tiketi kwa mechi ijayo ya CHAN 2024 kati ya Kenya na Zambia kwenye Uwanja wa Kasarani kufuatia machafuko na madai ya utapeli.

Haya yanajiri muda mfupi tu baada ya CAF kulitoza Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) faini ya Ksh 2.5 milioni kufuatia ukiukaji mkubwa wa usalama wakati wa mechi ya ufunguzi ya CHAN 2024 kati ya Kenya na DR Congo kwenye Uwanja wa Kasarani Agosti 3, 2025.

CAF imetaja ukiukwaji mkubwa wa usalama uliotatiza mchezo wa Harambee Stars dhidi ya Morocco Jumapili, 10 Agosti 2025, kuwa sababu kuu ya uamuzi wa kupiga marufuku uuzaji wa tiketi.

Matukio hayo wakati na kabla ya mechi hiyo ni pamoja na geti lililovunjwa, kuingia kwa mashabiki bila tiketi, kujaza kupita uwezo, uvamizi katika eneo la wanahabari na matumizi ya mabomu ya machozi.

Katika lango la 11, mkanyagano mkubwa ulitokea, na kuhatarisha maisha ya mashabiki kutokana na msongamano wa watu na ukosefu wa udhibiti. Baadhi ya watu pia waliingia katika eneo ya lililokatazwa na kukiuka itifaki za usalama.

Pikipiki iliyokuwa nje ya uwanja ilinaswa ikipita kwa hatari miongoni mwa mashabiki waliokuwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani.

Mlinzi wa binafsi wa pia alidaiwa kumvamia mfanyakazi wa CAF na mwakilishi wa wafadhili.

Kamati za nidhamu na usalama za CAF zinachunguza na zitaamua hatua zinazofuata.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment