Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imesema raia wa Malawi na Zambia, sasa watatakiwa kulipa dhamana ya hadi dola za Marekani elfu 15 ili kuingia kwenye taifa hilo kwa viza ya biashara au utalii.

Uamuzi huu wa Marekani, utaanza Agosti 20 kama sehemu ya mradi wa majaribio wa mwaka mmoja unaolenga kupunguza idadi ya watu wanaokaa kwenye taifa hilo zaidi ya muda waliopewa.
Dhamana hii itarejeshwa ikiwa mwombaji atatii masharti ya viza, lakini fedha yake haitarudishwa ikiwa mwombaji atasalia nchini humo hata baada ya tarehe ya mwisho ya hati inayomruhusu kukaa.
Malawi na Zambia ni miongoni mwa mataifa maskini yaliyo kusini mwa Afrika na ni raia wachache tu wanaotembelea Marekani kila mwaka.
Maafisa wa Marekani wanasema mradi huu ni “nguzo muhimu ya sera ya kigeni ya Utawala wa Trump kulinda Marekani dhidi ya tishio la wazi la usalama wa taifa linalotokana na watu wanaoamua kukaa kupita muda walioruhusiwa kisheria.
Katika miezi ya hivi karibuni, Rais wa Marekani Donald Trump ametekeleza masharti magumu ya viza kwa nchi nyingi, hasa barani Afrika, wakati huu akiongeza kasi ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.