Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa “Difficult Conversation” yaani mazungumzo magumu.
Haya ni yale mambo ambayo kama ungepewa fursa ya kuchagua kuyazungumza ama la, basi ungeyakwepa kabisa.
Ni yale mambo ambayo, unatamani kama yasingetokea na usingehusika nayo kabisaaa.
Inawezekana ni kwenye mahusiano na mtu unayempenda.
Kuna jambo lazima lizungumzwe ili maisha ya endelee na ubakie na amani yako ya kudumu.
Inawezekana ni kukiri jambo fulani ambalo umekuwa unalificha kwa muda mrefu.
Inawezekana ni kuomba msamaha au kuuliza kitu ambacho unahisi kinaendelea.
Kuna eneo unatakiwa uvunje ukimya.
Ila kila ukitaka kuchukua hatua, unaona uzito na unapata hofu.
Inawezekana ni kuhusu kazi yako, kuna jambo ambalo inabidi “umface” boss wako ila unaghairisha kila siku.
Kila ukijipanga, unaghairisha.
Inawezekana kuna mtu anakuingiza kufanya kitu kisicho sahihi na unatamani kumwambia ila kila ukitafakari, unapata hofu na unakaa kimya.
Matokeo yake, unazidi kukosa amani na unazidi kuingizwa katika kufanya ambacho hautaki.
Dawa ya mazungumzo magumu ni kuwa tayari kukabiliana nayo.
Chukua hatua.
Leo, muombe Mungu akupe HEKIMA na NGUVU ya kuyakabilia.
Nakuombea UJASIRI unapochukua HATUA leo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.