Je Unaongeza Ubora?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Njia nzuri ya kupanda juu zaidi ya ulipo leo ni kuongeza UBORA wa unachokifanya sasa hivi…

Moja Ya changamoto ya watu wengi ni kuishi wakiendelea KUTAMANI KIKUBWA ZAIDI huku WAKIDHARAU KIDOGO WALICHONACHO.

Yaani, mtu badala ya kufanya kwa BIDII na UAMINIFU katika NAFASI aliyonayo Leo, kila siku ANAHISI kuwa atafanya vizuri Kama ATAPEWA NAFASI KUBWA ZAIDI.

Nafasi uliyonayo na leo ni fursa ya kukusaidia kupanda Juu, usipoitumia vizuri utadumaa hapo hapo.

Badala ya kuendelea kulalamika kuwa UNALIPWA KIDOGO, badala ya kuendelea kutaka UPEWE CHEO KIKUBWA hadi unapiga wengine MAJUNGU, weka bidii kuonyesha kuwa UNASTAHILI KIKUBWA kupitia MATOKEO YA KAZI YAKO.

Fanya vitu kwa namna ambayo kila mtu ataona UMEKUA MKUBWA kuliko NAFASI au FURSA uliyonayo sasa hivi.

Njia nzuri ya KUKUA katika unachofanya SIO KUTUMIA FITNA na KUWACHAFUA WENGINE WALIOKO JUU YAKO bali ni wewe KUFANYA KWA UBORA SANA katika nafasi ndogo uliyopo hadi watu waone UNASTAHILI kupewa KIKUBWA SANA.

Kabla haujasema HAWAKUONI, jichunguze, Adui wa kwanza wa KUPANDA KWAKO JUU ni wewe MWENYEWE.

Je,leo utafanya nini cha Tofauti kuonyesha kuwa UNASTAHILI nafasi KUBWA ZAIDI?

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment