Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu wote ambao Mungu anakuruhusu UFAHAMIANE nao kwa UKARIBU huwa kuna MAKUSUDI ndani yake.
Kwa kawaida yetu wanadamu huwa tunapenda kujifunza kupitia WEMA wa watu tu.
Lakini nimejifunza kuwa kuna wakati tunapata MASOMO MUHIMU…
…na MAKUBWA kupitia MAUMIVU tuliyoyapata kutoka kwa wale walio karibu yetu.
Usifanye kosa kubwa la KUCHUKIA mtu kwa sababu ya MAUMIVU…
…wengine ni WATUMISHI wa MUNGU walioletwa Kwako kukuandaa kwa ajili ya KESHO YAKO.
Badala ya kuwalaani na kuwasema vibaya kila wakati…
Badala ya kujutia kwa nini ulikutana na kufahamiana nao…
Amua kutafuta MASOMO makubwa uliyoyapata kupitia MUDA uliokuwa nao.
Kuna watu kwa sababu ya walichokufanyia imekufundisha KUTHAMINI UPENDO unaopewa na wengine…
Kuna wengine kwa sababu ya uliyoyapitia wamekupa UMAKINI ZAIDI.
Kuna wengine walikuja kukuonesha na kukuonjesha uzuri wa kitu ambacho hukuwahi kufikiria kuwa kipo…
…walikuja kubadilisha mtazamo wako.
Hakuna mtu mbaya ambaye HAKUACHII SOMO la kukusaidia.
Badala ya kuendelea kuusema ubaya wake…
…pata Faida ya kujifunza ili ikusaidie mbele ya safari.
Appreciate the lessons!
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.