Hatua 3 Muhimu Unazotakiwa Kuchukua Ili Kuwa na Ujasiri Wa Kudumu…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Jipe Ujasiri Na Ufuate Cheo Chako

ii. Kabiliana Na Jitu Lako Leo

iii. Jenga Ujasiri Kuchukua Hatua Hii Leo

Katika Makala Hii Tutazungumzia Hatua ya Kwanza

– Jipe Ujasiri Na Ufuate Cheo Chako……..

Siku moja rafiki yangu alinipigia simu akaniambia…

…”sitapatikana hewani kwa muda kwa sababu naenda Monduli kusomea ngazi nyingine ya cheo jeshini”.

Baada ya kumuuliza maswali kadhaa nikagundua kuwa…

…ili apate cheo cha ziada ni lazima akajifunze vitu vya ziada na afanye mazoezi ya ziada.

Hata kama ni mtii, anamcha Mungu ila asipokuwa tayari kwa mafunzo ya ziada atabakia hivyo hivyo.

Hii ilimaanisha kutengwa na familia yake kwa muda mrefu.

Na pia kutoishi maisha aliyoyazoea.

Bali aanze kufuata taratibu na ratiba za mazoezi na mafunzo.

Ili uwe zaidi ya watu wa kawaida inakulazimu kufanya kitu kisicho cha kawaida.

Na wakati mwingine kufuata ratiba ambazo sio za kawaida na kujitenga kwa muda.

Kupanda nafasi ya juu katika kile unachofanya…

Ili upate faida zaidi…

Upate mshahara zaidi…

Upanuke zaidi…

Ukubalike na wengi zaidi inawezekana.

Ila swali la msingi ni…

Je, uko tayari kwenda Monduli?

Monduli yako inaweza kuwa ni…

Kuongeza ujuzi zaidi…

Kuacha tabia zinazokufelisha…

Kupunguza matumizi…

Kuongeza kisomo…

Kusoma vitabu zaidi…

Kuepuka baadhi ya marafiki n.k.

Ukiwa mtu wa kusema maneno tu…

“Nina malengo makubwa ila hauko tayari kuwekeza kwa kiwango cha ziada..

…hautapata matokeo unayoyataka”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment