Trump atishia kupunguza makataa ya siku 50 kwa Putin ya kufikia makubaliano ya Ukraine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mwandishi wa habari amebadilisha mazungumzo na kuuliza kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine, ambapo Trump alisema yeye na Rais wa Urusi Vladimir Putin wamekaribia kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano mara tano.

“Nimezungumza na Rais Putin sana, nimeelewana naye vizuri sana,” anasema, lakini akaongeza kuwa Putin “anatoka hapa na kuanza kurusha roketi katika jiji fulani, kama Kyiv, na kuua watu wengi katika nyumba ya wazee au popote pale, kisha miili inatapakaa barabarani”.

Trump alisema “amesikitishwa sana na Putin”, akiongeza kuwa anaweza kupunguza siku 50 alizompa rais huyo kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

“Nitapunguza hizo siku 50 nilizompa, kwa sababu nadhani nimeshajua jibu lake litakuwa lipi,” alisema.

Je, makataa ya siku 50 ya Trump kwa Putin yalikuwa yapi?

Tarehe 14 Julai, wakati wa mkutano katika Ikulu ya Marekani na mkuu wa Nato Mark Rutte, Trump aliahidi ushuru mkubwa kwa washirika wa kibiashara wa Urusi ikiwa Putin hataafikiana na Ukraine.

Rais wa Marekani alisema atatekeleza ushuru wa ziada wa 100% ikiwa hakutakuwa na makubaliano ndani ya siku 50.

Hii inamaanisha kuwa nchi yoyote ambayo inaendelea kufanya biashara na Urusi itakabiliwa na ushuru mkubwa wa kuuza bidhaa zao kwa Marekani, ripota wa biashara Dearbail Jordan alieleza.

Ingawa Urusi tayari inakabiliwa na vikwazo vingi katika nchi za magharibi, bado inafanya biashara na mataifa mengi, ikiwa ni pamoja na India na China.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment