“Niko Kwenye Mchakato”

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maalumu Kwa Wote Mnaokumbana Na Vikwazo Kila Kukicha…

Hebu anza kwa kujiambia “Niko Kwenye Mchakato”

Kila mtu anaweza kupata sababu ya kwa nini ni ngumu kwake kufanikiwa.

Kuna ambaye alikanwa na Baba yake…

…akalelewa na mama yake pekee kwenye mazingira magumu.

Huyu mwingine alishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada.

Kuna mwingine ambaye amejaribu mara kadhaa…

…ila kila wakati anapoteza mtaji.

Na huyu atasema ametokea familia ya kimaskini…

…na ni ngumu kwake kufanikiwa.

Ukweli ni kuwa, hakuna ambaye hawezi kuwa na…

…sababu ya kutofanikisha malengo yake.

Kwenye maisha ni lazima uamue kati ya haya mawili;

Changamoto ulizopitia/ulizonazo ziue ndoto zako zote au

Upambane na changamoto zinazokukabili na baadaye zitumike Kama ushuhuda wa ushindi.

Mungu ameruhusu changamoto zije kwa sababu anataka kuwathibitishia wengine kupitia wewe kuwa…

…pamoja na changamoto bado mtu anaweza kuinuka.

Yaani, wewe ni mwakilishi wa washindi wanaotengenezwa hapa duniani…

…ili wengine wasikate tamaa.

Uko kwenye mchakato.

Unachopitia unaweza kukishinda, usifunge ukurasa, bado una nafasi.

Nakukumbusha, Uko kwenye mchakato, usiishie Njiani.

Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu comment maneno “Niko Kwenye Mchakato”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment