Maumivu ni sehemu ya kukua-unapofuatilia Ndoto yako.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maumivu ni sehemu ya kukua. Unapofuatilia NDOTO YAKO Kuna wakati utapitia maumivu ambayo kwa haraka sana akili yako itakuambia kuwa njia rahisi zaidi ya KUYAEPUKA ni KUACHA unachokifanya. Hata hivyo imethibitika kuwa kila maumivu unayokutana nayo kwenye mchakato wa kupambania malengo yako, yana FAIDA ndani yake.
.
Maumivu ni njia ya kukuonyesha kuwa unakaribia KUVUKA KIWANGO cha kawaida. Ukiongea na wakimbiaji watakuambia kuwa wanaposikia maumivu MAKALI ndipo wanatakiwa KUJILAZIMISHA kuongeza bidii,akina mama watakuambia kuwa wanaposikia uchungu wakati wa ujauzito ndipo wanapotakiwa kuongeza ujasiri na kusukuma ili wapate mtoto waliyekuwa wanamtarajia kwa muda mrefu.
.
Jambo mojawapo unalotakiwa kulifahamu ni kuwa:Kwenye maisha wanaoshinda na kufanikiwa sio wenye NGUVU,AKILI au UWEZO mkubwa bali nyongeza ya ziada katika hayo ni kuwa na uwezo wa KUVUMILIA hadi mwisho.Uwezo wako wa kuwa na ujasiri wa kuendelea katikati ya maumivu kwa sababu UNAAMINI kuwa GHARAMA ya MAUMIVU unayopitia ni NDOGO SANA ukilinganisha na FAIDA UTAKAYOPATA baada ya KUSHINDA.
.
Kumbuka hakuna ANAYESHINDA kwa KUKATA TAMAA kwa sababu ya MAUMIVU anayopitia.Kama unataka kushinda ni lazima UWE NGANGARI kwa muda MREFU zaidi ya muda ambao MAUMIVU YAKO YATADUMU.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment