Kuna watu watasahau wema uliowafanyia…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wapo watu wengi ambao wanaishi katika maumivu kwa sababu waliwahi kumtendea mtu/watu mema ila hawakulipwa mema au walilipwa ubaya.

Nimeshakutana na watu ambao wamejinyima kwa muda mrefu ili wwawasaidie WAZAZI wao, ila wanambuliwa kutukanwa na kusemwa vibaya na haohao wazazi.

Haujawahi kukuta mtu anajinyima sana kwa ajili ya ndugu zake na mwisho wa siku, hao ndugu ndio wanaoongoza kumsema vibaya kwa watu?

Wakati mwingine hata kwenye mahusiano, yaani mtu unajitoa na kujinyima ila mwishoni unaishia kubebeshwa lawama.

Wapo ambao wamejitoa sana kwenye ofisi, mwisho wakafukuzwa kwa aibu.

Iko hivi, usiweke MATARAJIO makubwa sana kwa watu baada ya kuwatendea mema. Wengine HAWATAKUMBUKA na HAWATAKULIPA kabisa.

Fanya ukijua kuwa, MALIPO yako yatatoka kwa MUNGU na anaweza kutumia watu wengine TOFAUTI na wale ambao ULIWAFANYIA.

Kama umependa makala hii tafadhali share na wengine.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment