USIENDELEZE MAUMIVU YA KUKATALIWA…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna watu wengi sana ambao kinachowatesa sio KUKATALIWA bali ni kuendeleza maumivu ya kukataliwa.

Kwenye maisha kila mtu huwa anapitia hali ya kukataliwa, unataliwa uipokee na UIKABILI.

Kuna watu wamewahi kukataliwa kwenye kuomba kazi, wengi wamekataliwa kwenya mahusiano na wengine wamekataliwa hadi na wazazi wao.

Iko hivi, maumivu hayatokani tu na kukataliwa, bali hasa yanatokana na UNAVYOJITAFSIRI baada ya kukataliwa.

Wengi wakishakataliwa, huwa wanajiona HAWAFAI na wao si KITU KABISA. Wengine hadi wanaacha KUJIPENDA tena.

Kumbuka, Kukataliwa ni TUKIO LA MARA MOJA ila unavyojiona baada ya kukataliwa ndio kitu cha MUHIMU.

Usiruhusu mtu mmoja aliyekukataa akufanye upoteze thamani yako, wako wengi wanakusubiri wakupe thamani UNAYOSTAHILI.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment