Marekani na Israel yashutumu mpango wa Ufaransa wa kutambua serikali ya Palestina

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa uamuzi wa Ufaransa kulitambua rasmi taifa la Palestina ni “kuzawadia ugaidi”, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akisema hatua hiyo “ni ya kutojali”.

Ufaransa ilitangaza kuwa italitambua rasmi taifa la Palestina mnamo mwezi Septemba hatua iliyopokelewa kwa shangwe na maafisa wa Palestina.

Siku ya Alhamisi, wapatanishi wa Israel na Marekani katika mzozo wa Gaza waliamua kuondoka kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano yaliyokuwa yakifanyika huko Qatar, huku Washington ikimshtaki Hamas kwa “kutojitolea kwa nia njema”.

Hamas inasema ilishangazwa na madai hayo huku chanzo cha Israel kikisisitiza kuwa “hakuna kilichoporomoka” katika mazungumzo hayo.

Wakati huo huo, hali ya kibinadamu katika eneo la Gaza inaendelea kuwa mbaya tena kwa kasi mno. Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Palestina (UNRWA) linaonya kwamba mtoto mmoja kati ya watano katika mji wa Gaza ana utapiamlo – kaskazini mwa eneo hilo – na kwamba visa hivyo vinaongezeka kila siku.

Israel na Hamas wote wanalaumiana kwa hali hiyo, huku mashirika ya misaada yakiwa yanatoa wito kwa Israel kuruhusu misaada zaidi kuwafikia watu katika eneo hilo, wakionya juu ya baa kubwa la njaa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment