Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wanawake watano wa Australia ambao walivuliwa nguo na kuchunguzwa katika uwanja wa ndege wa Doha wameshinda haki ya kushtaki Qatar Airways baada ya kukata rufaa.
Wanawake hao waliamuriwa kushuka kwenye ndege na kukaguliwa iwapo walikuwa wamejifungua baada ya mtoto kupatikana akiwa ametelekezwa kwenye pipa la uwanja wa ndege mnamo mwaka 2020 – tukio ambalo lilizua ghadhabu duniani.
Jaji wa Australia mwaka jana aligundua shirika la ndege linalomilikiwa na serikali halingeweza kufunguliwa mashitaka chini ya sheria zinazosimamia usafiri wa kimataifa, na akasema tukio ambapo wafanyakazi wake waliingilia kati kiasi hicho lilikuwa “lisilo fikirika, lisilo na maana, fedheha, tukio lisiloweza kuamini kama linaweza kutokea, [na] uchungu”.
Wanawake hao walikata rufaa, huku majaji wa mahakama wakisema kuwa hakimu mkuu alikosea kutupilia mbali kesi hiyo.
Wanawake hao watano walifungua kesi mwaka 2021, dhidi ya Qatar Airways, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Qatar na waendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, kampuni inayoitwa Matar.
Walitaka kulipwa fidia kutokana na madai ya “kugusana kinyume cha sheria” na kifungo cha uwongo ambacho kilisababisha athari za afya ya akili ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo na kiwewe. Abiria wengine ambao walichunguzwa – ni pamoja na kutoka Uingereza na New Zealand – ambao hawakuwa sehemu ya kesi hiyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.