Timu ya IAEA itazuru Iran lakini haitafika katika vituo vya nyuklia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Kazem Gharibabadi, amesema kuwa, ujumbe wa masuala ya kiufundi kutoka Shirika la Nishati ya Atomiki (IAEA) hivi karibuni watazuru Tehran, lakini hawataruhusiwa kutembelea vituo vya nyuklia vya Iran.

Bw. Gharibabadi, ambaye yuko New York, alisema kuwa Iran imekubali ziara ya timu ya kiufundi ya IAEA mjini Tehran katika muda wa wiki mbili hadi tatu zijazo.

Shirika la habari la Reuters limenukuu Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki likisema kwamba Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Rafael Grossi, “anafanya mazungumzo kikamilifu na pande zote zinazohusika na suala la nyuklia ya Iran.”

Inaonekana kuwa ziara hii imepangwa kwa muda kabla ya mkutano wa robo mwaka wa Baraza la Magavana, ambao umepangwa kushughulikia suala la nyuklia ya Iran tena mnamo mwezi Septemba.

Bwana Gharibabadi alisisitiza kuendelea kwa mpango wa nyuklia wa Iran na kuonya juu ya uchochezi unaofanywa na serikali za Ulaya na kuwa kurejeshwa kwa vikwazo na Baraza la Usalama dhidi ya Iran kutakabiliwa vikali nan chi hiyo.

Serikali tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeipa Iran hadi mwisho wa mwezi wa Agosti, takriban wiki tano kutoka sasa, kuingia katika makubaliano mapya ya nyuklia, au nchi hizi zitaanzisha tena vikwazo vya Baraza la Usalama.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi hapo siku za nyuma, aliwahi kusema kwamba maombi ya shirika la IAEA yatapitiwa upya hatua kwa hatua na Baraza Kuu la Usalama la Taifa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment