Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini wameomba msamaha kwa mwanamke aliyepatikana na hatia kwa kujitetea wakati wa shambulio la ukatili wa kingono zaidi ya miaka 60 iliyopita.
Choi Mal-ja alihukumiwa kifungo cha miezi 10 jela na hukumu nyingine ya miaka miwili iliyocheleweshwa, kwa kumng’ata sehemu ya ulimi mshambuliaji wake alipodaiwa kujaribu kumbaka mwaka 1964, alipokuwa na umri wa miaka 18.
Akihamasishwa na vuguvugu la #MeToo nchini humo, Bi Choi, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 78, amefanya kampeni kwa miaka mingi kutaka hukumu yake ibatilishwe.
Kesi yake ilianza kusikilizwa tena katika jiji la Busan siku ya Jumatano, ambapo waendesha mashtaka waliomba radhi na kuomba mahakama ifutilie mbali hukumu yake ya hatia.
“Kwa miaka 61, serikali ilinifanya niishi kama mhalifu,” Bi Choi aliambia wanahabari nje ya mahakama kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Alisema anatumai vizazi vijavyo vinaweza kuishi maisha ya furaha bila unyanyasaji wa kijinsia.
Mwanzoni mwa kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Busan Jeong Myeong-won alisema “tunaomba radhi”.
“Tumesababisha kwa Choi Mal-ja, mwathirika wa uhalifu wa ngono ambaye alipaswa kulindwa, maumivu na uchungu usioelezeka.”
Uamuzi wa mwisho umepangwa kufanyika Septemba 10, huku waangalizi wa kisheria wakitarajia mahakama kubatilisha hukumu ya Bi Choi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.