Wanandoa wa Uingereza wanaoshikiliwa na Taliban ‘wanaweza kufa gerezani,’ mtoto wao aonya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wenza

Mtoto wa wanandoa wa Uingereza waliozuiliwa na kundi la Taliban miezi mitano iliyopita ameiambia BBC kuwa anahofia kuwa huenda wakafia gerezani.

Peter Reynolds, 80, na Barbie, 76, walikamatwa tarehe 1 Februari walipokuwa wakirejea nyumbani kwao katika jimbo la kati la Bamiyan, Afghanistan.

Haijulikani hasa kwa nini walizuiliwa. Mtoto wao wa kiume Jonathan Reynolds alisema afya yao ilikuwa ikizorota kwa kasi, huku baba yake akipata degedege kubwa na mama yake “amekufa ganzi” kutokana na upungufu wa damu na utapiamlo.

Waziri wa mambo ya nje wa Taliban alisema wanapatiwa matibabu na kwamba “juhudi zinaendelea ili kuwaachilia huru, lakini mchakato huo haujakamilika”.

“Haki zao zote za kibinadamu zinaheshimiwa,” Amir Khan Muttaqi aliwaambia waandishi wa habari mjini Kabul siku ya Jumatano, na kuongeza kuwa wawili hao walikuwa “na mawasiliano ya mara kwa mara” na familia.

Umoja wa Mataifa ulionya Jumatatu kwamba wanandoa hao wanaweza kuangamia “katika hali hiyo ya kudhalilisha” ikiwa hawatapata huduma ya matibabu mara moja, ikiita kuzuiliwa kwao “kukosa ubinadamu”.

Bw Reynolds alisema imekuwa ” hali ya kuhuzunisha na ya kusikitisha” kwa miezi mitano akingojea kuachiliwa kwa wazazi wake, ambao waliishi Afghanistan kwa miaka 18, ambapo walikuwa na uraia na waliendesha miradi ya elimu.

Moja ya miradi hii ilihusisha kutoa mafunzo kwa wanawake na watoto na inaonekana ilikuwa imeidhinishwa na mamlaka za mitaa, licha ya Taliban kupiga marufuku elimu kwa wasichana wenye umri wa zaidi ya miaka 12 na kutoruhusu wanawake kufanya kazi.

Bw Reynolds alisema wazazi wake walikuwa wakishikiliwa katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na gereza lenye ulinzi mkali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment