Trump asema Marekani imefikia makubaliano ya kibiashara na Japan

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba

Rais Donald Trump anasema Marekani imekubali makubaliano “mkubwa” ya kibiashara na Japan, mojawapo ya washirika wakubwa wa kibiashara wa nchi hiyo.

Japan imekubali kuwekeza $550bn (£407bn) nchini Marekani huku bidhaa zake zinazouzwa Marekani zikitozwa ushuru wa 15% zitakapofika nchini, chini ya ushuru wa 25% ambao Trump alitishia.

Trump alisema kwenye mitandao ya kijamii kuwa Japan itafungua uchumi wake kwa bidhaa za Marekani, yakiwemo magari, malori, mchele na baadhi ya bidhaa za kilimo.

Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba alilipokea tangazo hilo kwa mikono miwili, akisema ni “idadi ya chini zaidi kufikia sasa kati ya nchi zilizo na ziada ya biashara na Marekani”.

“Nimesaini mkataba mkubwa zaidi wa kibiashara katika historia, nadhani labda mkataba mkubwa zaidi katika historia na Japan,” Trump alisisitiza katika hafla ya White House Jumanne jioni.

“Walikuwa na watu wao wakuu hapa, na tuliifanyia kazi kwa muda mrefu na kwa bidii. Na ni mpango mzuri kwa kila mtu. Siku zote nasema lazima uwe bora kwa kila mtu. Ni mpango mzuri,” aliongeza.

Ishiba alisema Jumatano makubaliano hayo yatamaanisha ushuru wa Marekani kwa magari kwa sehemu zitapunguzwa hadi 15% kutoka 25%.

Robo ya mauzo ya nje ya Japan ya Marekani yanatokana na sekta yake muhimu ya magari, ambayo inachangia karibu 3% ya uchumi wake.

Mnamo 2019, thamani ya usafirishaji wake wa magari ilikuwa $410bn (£300bn), kulingana na Ofisi ya biashara ya kimataifa ya Marakani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment