Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hakuna ambaye anafurahia kupitia hali ngumu ya maisha, ila hakuna anayeweza kuishi bila kupitia nyakati ngumu.
Inawezekana kabisa kwa sasa ukafikiria kwamba ni wewe peke yako ndiye ambaye unapitia hali ngumu, sio kweli, kuna wengi wanapitia pia na wengine ni ngumu zaidi yako.
Kila unachopitia leo, Mungu amekiruhusu kwa sababu kina faida kwenye maisha yako.
Kuna magumu unapitia ili ujengewe STAMINA na MISULI ya kukusaidia kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yako.
Yaani, kuna UKUBWA uko mbele yako na kutakuwa na changamoto KUBWA zinakusubiri, ili uzishinde inabidi UANDALIWE MAPEMA.
Hii ndio maana, usiwe mtu wa KUZIKIMBIA CHANGAMOTO bali uwe mtu wa KUKABILIANA nazo.
Kumbuka: Kuna wakati MUNGU hatajibu maombi ya changamoto KUONDOLEWA bali ATAKUPA NGUVU za kukabiliana nazo.
Nakuombea USHINDI!
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.