JE, UNAONA GIZA MBELE YAKO?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu wengi sana wamepoteza mwelekeo wa maisha yao baada ya kukutana na hali iliyoleta GIZA kwenye maisha yao.

Yaani, walikutana na kitu kilichowafanya WATOE MACHOZI, au wakate TAMAA kabisa.

Kuna watu baada ya KUPOTEZA KAZI au MTAJI wa biashara, wakaanza kuona giza.

Kuna wengine baada ya kupoteza MAHUSIANO yao walianza kuona giza.

Wapo ambao baada ya KUFELI shule au kufariki mtu waliyempenda sana au kumtegemea, walianza kuona GIZA.

Usisahau kuwa hii ni hatua ya maisha. Ni kweli imekufanya USIMAME ila usiruhusu ikufanye UFIKE MWISHO.

Kama leo unapitia hali ya namna hii, nakuombea kwa Mungu akusaidie upate nguvu za kuinuka na kuanza upya.

INUKA, KESHO YAKO INANG’ARA SANA.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment