Watu 19 wafariki baada ya ndege ya jeshi la anga kuanguka Bangladesh

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Takribani Watu 19 wamefariki dunia na wengine 164 kujeruhiwa baada ya ndege ya mafunzo ya jeshi la anga ya Bangladesh kuanguka katika shule moja katika mji mkuu, Dhaka.

Picha kutoka Shule ya Milestone iliyopo katika kitongoji cha kaskazini cha Uttara zinaonyesha moto mkubwa na moshi ukifuka baada ya ndege hiyo kugonga jengo la orofa mbili.

Vikosi vya kijeshi vilisema kwenye taarifa kwenye Facebook kwamba ndege ya F-7 ilipata hitilafu ya kiufundi baada ya kupaa kwa ajili ya mazoezi baada ya saa 13:00 za saa za huko (07:06 GMT).

Rubani alikuwa miongoni mwa waliofariki, jeshi la anga liliongeza kusema.

Zaidi ya watu 50, wakiwemo watoto na watu wazima, walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha ya moto, daktari katika Taasisi ya Kitaifa ya Upasuaji alisema.

Umri wa wanafunzi wanaohudhuria shule hiyo ni kati ya miaka minne na 18.

Mwalimu wa shule hiyo, Rezaul Islam, aliiambia Idhaa ya Bangla ya BBC kwamba aliona ndege ikigonga jengo hilo “moja kwa moja”.

Mwalimu mwingine, Masud Tarik, aliiambia shirika la habari la Reuters kwamba alisikia mlipuko: “Nilipotazama nyuma, niliona moto na moshi … Kulikuwa na walezi wengi na watoto hapa.”

Mwanafunzi mmoja alisema kuwa aliona ndege ikigonga jengo “mbele ya macho yangu”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment