Maandamano Kenya: Boniface Mwangi afutiwa mashtaka ya ugaidi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

k
Maelezo ya picha,Boniface Mwangi ni mwanaharakati maarufu na amehusika katika maandamano mengi

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchni Kenya imetupilia mbali mashtaka yanayohusiana na ugaidi yaliyofungiliwa dhidi ya mwanaharakati Boniface Mwangi.

Mwangi sasa anakabiliwa na mashtaka mawili, ikiwa ni pamoja na kumiliki silaha bila kibali na kupatikana na sumu pamoja na vitoa machozi.

Alikana shtaka hilo na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni moja za Kenya.

Kukamatwa kwake kumelaaniwa, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakikosoa kuwa ni kwa lengo la kukandamiza sauti za upinzani.

Mwanaharakati huyo amekanusha tuhuma hizo, akisema katika chapisho kwenye X: “Mimi sio gaidi.”

Tuhuma zinazohusishwa na maandamano ya Juni 25, kulingana na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) inayofadhiliwa na serikali.

Watu 19 walikufa wakati waandamanaji walipopambana na polisi. Mamia pia walijeruhiwa na mali na biashara kuharibiwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen ameeleza maandamano hayo kama “ugaidi uliojificha kama upinzani” na “jaribio lisilo la kikatiba” la kuiangusha serikali.

Watu 38 zaidi waliuawa katika maandamano yaliyofuata mapema mwezi huu, KNHCR imesema.

Tangu Juni mwaka jana, zaidi ya watu 100 wameuawa katika wimbi la maandamano ya kupinga serikali, huku polisi wakituhumiwa kutumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment