‘Gangsta Debbs’ – Mongwe aliyetumia familia yake kuendesha biashara ya madawa ya kulevya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mapema asubuhi ya Aprili 2023 maafisa wa ujasusi walimtazama mwanamke akipakia masanduku kwenye gari la kukodi kwenye duka la bidhaa za reja reja karibu na bandari ya Harwich huko Essex.

Walipata taarifa kuhusu gari lililokuwa limesafiri kutoka Islington usiku huo.

Gari hilo liliendeshwa kuelekea Ipswich, ambapo mwanamke huyo alikabidhi begi zito la nguo kwa mtu asiyejulikana.

Hakuonekana kama mtu ambaye ungetarajiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya – wakili wake wa utetezi alisema “bila shaka alitajwa kama mtu ambaye hangevutia macho”.

g
Maelezo ya picha,Deborah Mason alijiita Gangsta Debbs. Binti yake, Demi Bright, alihifadhi nambari ya mamake kwenye simu yake kama ‘Queen Bee’.

Mwanamke huyo alikuwa Deborah Mason, anayejulikana kwa familia kama Gangsta Debbs au Malkia Bee: bibi na mama mkuu wa familia ya uhalifu ambayo ilifanya kazi kote kusini mashariki mwa Uingereza.

Mason alikuwa amewaajiri watoto wake wanne, dada yake na watu wengine wa karibu wa familia kusaidia usambazaji wa Kokeini kote nchini – kufadhili maisha ya kifahari ambayo yalijumuisha bidhaa za mbuni wa Gucci zilizonunuliwa kwa paka wake na birika la kifahari la Bugatti la pauni 192.

Siku ya Ijumaa, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 65 alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kula njama ya kusambaza dawa za Daraja A katika Mahakama ya Woolwich Crown.

Wengine katika genge hilo walipata hukumu ya vifungo vya kati ya miaka 10 na 15 kwa mashtaka sawa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment