Maeneo 4 Muhimu Ya Kumpa Uongozi Mume Wako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Maamuzi Yanayohusu Mwelekeo Wako

ii. Maamuzi Yanayohusu Familia Yenu

iiii. Maamuzi Yanayohusu Watoto Wenu

iv. Maamuzi Yanayohusu Watu Muhimu Kwenu (Wazazi, Ndugu N.k)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Eneo La Nne

– Maamuzi Yanayohusu Watu Muhimu Kwenu (Wazazi, Ndugu N.k)

Kwenye familia zetu za kiafrika ndugu ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku.

Hakikisha maamuzi muhimu unayoyafanya yanayohusisha ndugu zako unamtaarifu pia.

Usifanye maamuzi ya kuleta ndugu wa kuishi naye bila kujadiliana naye.

Usianze kujengea wazazi wako nyumba bila kumtaarifu.

Usilipie ndugu zako ada kwa siri bila kuzungumza naye…

…kumpa mtaji mkubwa n.k

Kumbuka hili siku zote, hata kama wewe ndio unagharamia kila kitu…

…hakikisha jambo hilo halimny’ang’anyi nafasi yake ya kukuongoza.

Nafasi ya uongozi kwa mwanaume ni moja ya kitu muhimu sana kinachoweza kumfanya akusapoti au la…

…hata siku moja usimfanye ajihisi anaitetea kwa nguvu au ahisi kuwa amenya’ang’anywa nafasi yake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment