Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ndio Yuko Kimya, ILA Sio Kwamba Ana Kiburi, La Hasha…
Ni kwa sababu amefikia kiwango cha mwisho cha maumivu na hawezi kuongea tena.
Kuna watu tuko nao, marafiki, wenzi, watoto, wafanyakazi wenzetu n.k
Kuna wakati unawaona wako kimya, usihitimishe kuwa hawataki kuongea.
Kuna wengine, yaani nguvu zote zimewaishia kabisa na hawawezi hata kuongea kitu.
Kuna watu wanapitia maumivu ya mahusiano.
Wengine wamefanyiwa vitu ambavyo hawawezi kuviongea.
Wapo ambao wamesingiziwa na jamii imeshawahukumu n.k
Ukimuona unayempenda amekuwa kimya usiseme “Hataki kuongea”.
Inawezekana kuna maumivu yanamla ndani kwa ndani na amekosa kabisa msaada.
Kwa unayempenda, ukiona amekuwa kimya basi usimpuuze.
Tafuta namna ya kumsaidia.
Usimlazimishe aongee, unaweza kutengeneza mazingira tu ya kupata muda naye.
Mtoe “out”.
Mpe zawadi.
Mtafute mara kwa Mara kumsalimia n.k
Akijihakikishia kuwa unamjali sana, basi ataanza kufunguka.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.