OMBA MUNGU AKUFUNGUE MACHO ILI UMTAMBUE MTU ALIYEBEBA KESHO KUBWA BILA KUJALI ALIVYO LEO.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hivi unajua unahitaji MACHO YA ZIADA kuona HATIMA KUBWA ya KESHO kwa MTU unayemfahamu leo ambaye bado ANAONEKANAWA KAWAIDA?

Baada ya Yesu kufikisha miaka 12, kutokana na taratibu za wayahudi ilibidi kwenda kumuweka wakfu hekaluni.

Sasa, kule HEKALUNI kulikuwa na mzee mmoja anaitwa SIMEONI.

Wakati wengine wote walimuona YESU ni kama mmoja wa watoto waloletwa na wazazi wao kama kawaida, SIMEONI alijua HATIMA kubwa ambayo YESU ameibeba, AKAITAMBUA na AKAISEMA (Luka 2:22-33).

Cha ajabu ni kuwa, hata WAZAZI wa YESU walishangaa sana MANENO ya Simeoni kuhusu mtoto wao, nao HAWAKUJUA sana UKUU WAKE.

Kwenye maisha, kuna watu wengi sana ambao MUNGU anaweza akawaleta kwako kwenye UDOGO WAO ila wamebeba KESHO KUBWA SANA.

Usipomuomba MUNGU AKUFUNGUE macho MAPEMA, unaweza KUPOTEZA WATU WAKUBWA wengi ambao kwa sasa wanaonekana kama ni wa KAWAIDA.

Muombe MUNGU, akufungue MACHO ili usipoteze watu ANAOKULETEA wakiwa wa kawaida ili akuunganishe nao kwa AJILI YA KESHO.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment