Uchaguzi mkuu wa urais nchini Cameroon kufanyika Oktoba 12 mwaka huu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Uchaguzi wa urais unaosubiriwa nchini Cameroon, umepangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Oktoba.

 Paul Biya- Rais wa Cameroon.
Paul Biya- Rais wa Cameroon. AP – Sunday Alamba

Tarehe hii imetangazwa na kiongozi wa muda mrefu rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 43.

Hata hivyo mpaka sasa, rais Biya hajathibitisha iwapo atawania tena uongozi wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati, kwa muhula wa nane.

Siku ya kufanyika kwa uchaguzi huo, imetangazwa wakati huu upinzani ukiwa umeendelea kugawanyika, bila ya kuwa na mgombea mmoja, ambaye anatarajiwa kupambana na rais Biya, ambaye uwezekano wa kuwania tena ni mkubwa.

Hata hivyo, chama tawala kinaonekana kugawanyika iwapo rais Biya aendelee kuungwa mkono, huku mshirika wake wa karibu Bello Bouba Maigari, Waziri Mkuu wa zamani, akijiuzulu na kutangaza mpango wa kuwania uongozi wa nchi hiyo.

Wale wanaotaka kuwania urais, wana hadi Julai 21 kuonesha nia yao kwa Tume ya Uchaguzi, akiwemo kiongozi wa upinzani Maurice Kamto, ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2018, aliibuka katika nafasi ya pili.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment