Congo yataka maelezo kutoka Uganda kuhusu kufunguliwa kwa mpaka wa Bunagana

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inataka maelezo kutoka kwa serikali ya Uganda, kuhusu kufunguliwa kwa mpaka wa Bunagana, katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23.

Waandamanaji wakizuiliwa na polisi walipojaribu kuandamana kuelekea mpaka na Rwanda, huko Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumatano Juni 15, 2022. (Picha ya AP/Moses Sawasawa)
Waandamanaji wakizuiliwa na polisi walipojaribu kuandamana kuelekea mpaka na Rwanda, huko Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumatano Juni 15, 2022. (Picha ya AP/Moses Sawasawa) AP – Moses Sawasawa

Kufuatia kikao cha Baraza la Mawaziri, Wizara ya Mambo ya nje, imetakiwa kutafuta majibu kutoka kwa serikali ya Uganda, ni kwanini mpaka huo ulifunguliwa tena wiki hii, bila ya kuwepo kwa maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mpaka wa Bunagana ulifunguliwa tena siku ya Alhamisi, na maafisa wa serikali ya Uganda, katika eneo hilo ambalo tangu mwezi Juni mwaka 2022 kwa sababu za kiusalama, lipo chini ya waasi wa M 23.

Ripoti zinasema, mpaka huo ulifunguliwa baada ya maagizo ya Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba baada ya maelekezo ya rais Yoweri Museveni, ili kufungua tena fursa hasa za kibiashara kati ya nchi hizo jirani.

Tangu kufungwa kwa mpaka wa Bunagana, wenyeji wa Bunagana kutoka pande zote mbili, kulisababisha ukosefu wa ajira na kuanza kusababisha umasikini kati ya raia wa kawaida.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment