Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jaji wa Marekani kwa mara nyingine amemzuia Rais Donald Trump kutekeleza agizo la rais la kukomesha uraia wa haki ya kuzaliwa kwa baadhi ya wakaazi wa Marekani huku pingamizi hiyo ya kisheria ikiendelea.
Jaji wa New Hampshire alitoa uamuzi wa kesi dhidi ya agizo la Rais Trump, na akasimamisha kwa muda agizo hilo la rais kutekelezwa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu la American Civil Liberty kwa niaba ya wazazi wahamiaji na watoto wao.
Uamuzi huo unatolea wiki kadhaa baada ya Mahakama ya Juu Zaidi kuanzisha ukomo wa jinsi na wakati maagizo ya mahakama yanatolewa na Mahakama ya Serikali Kuu.
Hata hivyo, uamuzi huo bado unawaruhusu kupitia njia fulani za kisheria.
Katiba ya Marekani inawahakikishia uraia wote waliozaliwa katika ardhi ya Marekani, lakini Trump ametaka kubatilisha haki hiyo kwa watoto wanaozaliwa na wahamiaji wasio na vibali na raia kutoka nchi za kigeni, kama sehemu ya msako dhidi ya wahamiaji haramu.
Kesi ya hiyo inalenga kupinga agizo hilo kama lenye madhara na kinyume na katiba, na hakimu aliamua kwamba inaweza kuendelea kwa niaba ya watoto wachanga ambao itawaathiri.
Kwa mara ya nyingine tena uamuzi huo pia unasimamisha agizo ambalo lilikuwa kipaumbele kwa Trump. Jaji ameipa serikali siku saba kukata rufaa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.