Mbinu Kumi Za Kupata Mtaji Wa Biashara Yako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Nguvu Zako

ii. Ujuzi

iii. Msaada

iv. Mkopo Wenye Masharti Nafuu

v. Kuuza Ulichonacho

vi. Mwekezaji

vii. Mahusiano Mazuri Na Kuaminika

viii. Vikundi Vya Kuweka Na Kukopa.

ix. Akiba Kutokana Na Kipato Chako Cha Sasa.

x. Kutumia Mashine/Vifaa Ulivyonavyo

Katika Makala Hii Tutazungumzia mbinu ya Tisa Ya kupata Mtaji

– Akiba Kutokana Na Kipato Chako Cha Sasa.

Unaweza kuanzisha biashara pia kwa kutumia kipato chako cha sasa kutokana na unachofanya.

Hivi karibuni nilikutana na dada aliyekuwa anafanya kazi za ndani akiwa na biashara yake.

Nilipomuuliza akanieleza kuwa, kwa sababu alikuwa na maono ya kuanzisha biashara, basi kwa kila pesa ambayo alikuwa analipwa alikuwa anaweka pembeni kiasi fulani kwa ajili ya kukusanya mtaji.

Inawezekana kwa sasa unafanya kazi usiyoipenda na tena wanakulipa kiasi kidogo sana cha pesa.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa, katika hicho kiasi kidogo unaanza kutenga pesa pembeni ya kujikusanyia mtaji wako.

Watu wengi ukiwaambia hivi, watakujibu kuwa hiyo pesa wanayopata haiwatoshi, sio kweli. Ukichunguza matumizi yako, utagundua kuna maeneo mengi ambayo unapoteza pesa yako.

Kama hautajibana na kutengeneza mpango wa wewe kutoka hatua uliyopo kwenda hatua nyingine basi itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa kuanzisha biashara.

Jibane na uteseke sasa hivi, ili baadaye uwe na maisha na mafanikio unayoyatamani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment