Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mazungumzo kati ya Israel na Hamas nchini Qatar kuhusu mpango mpya wa kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka yamekwama baada ya siku tatu za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, afisa wa Palestina ameiambia BBC.
Afisa huyo alisema mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na jinsi misaada itakavyosambazwa wakati wa usitishaji mapigano na uondoaji wa wanajeshi wa Israel.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anazuru Marekani na matumaini ya kufikiwa makubaliano yameongezwa kwani alikuwa na mkutano wa pili ambao haukutarajiwa na Rais Donald Trump siku ya Jumanne.
Mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff pia alisema kwamba alikuwa na matumaini ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku 60 mwishoni mwa wiki hii.
Mtazamo wa mikutano kati ya Trump na Netanyahu umetoa hisia kwamba kasi kuelekea makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza inaongezeka.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi, waziri mkuu wa Israel alisema mkutano wao wa hivi karibuni “ulilenga juhudi za kuwaachilia mateka wetu”. “Hatulegei, hata kwa muda, na hili linawezekana kutokana na shinikizo la kijeshi la askari wetu mashujaa.”
Aliongeza: “Tumedhamiria kufikia malengo yetu yote: Kuachiliwa kwa mateka wetu wote walio hai na waliokufa, na kuondolewa kwa uwezo wa kijeshi na kiutawala wa Hamas, na hivyo kuhakikisha kwamba Gaza haitakuwa tena tishio kwa Israel.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.