Familia zaingiwa wasiwasi kuhusu usalama wa Wahindi waliotekwa nyara nchini Mali

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kambi za kijeshi nchini Mali zilishambuliwa mara kadhaa mwezi uliopita

Wiki moja baada ya Wahindi watatu kutekwa nyara nchini Mali, familia zao zinasema bado hazina taarifa kuhusu waliko na zina wasiwasi kuhusu usalama wao.

Wizara ya mambo ya nje ya India ilisema watu hao, ambao walifanya kazi katika kiwanda cha saruji nchini Mali, “walichukuliwa kwa nguvu” na kundi la “washambuliaji wenye silaha” Jumanne iliyopita.

Serikali ya Mali bado haijasema lolote, lakini utekaji nyara ulifanyika siku ambayo kundi lenye uhusiano na al-Qaeda – Jama’at Nusrat al-Islam wal Muslimin (JNIM), lilidai kuwa limefanya mashambulizi kadhaa katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Kulingana na takwimu za serikali, Wahindi takribani 400 wanaishi Mali, nchi ambayo India imekuwa na uhusiano wa kibiashara nayo tangu miaka ya 1990.

Tukio la wiki iliyopita linakuja baada ya raia watano wa India kutekwa nyara nchini Niger, mwezi wa Aprili wakati wa shambulio la watu wenye silaha ambao pia waliwauwa wanajeshi kumi na wawili, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Hakuna taarifa kuhusu mahali walipo. Niger, Mali na Burkina Faso wanapambana na uasi wenye uhusiano na al-Qaeda na Islamic State (IS) ulioanza kaskazini mwa Mali mwaka 2012 na tangu wakati huo kuenea katika nchi jirani.

Mali ni taifa la nane kwa ukubwa katika bara la Afrika na lipo katika eneo la Sahel barani Afrika, ambalo Ripoti ya Kimataifa ya Ugaidi (GTI) ilieleza kuwa “kitovu cha ugaidi duniani” mapema mwaka huu.

Kanda hiyo inachangia “zaidi ya nusu ya vifo vyote vinavyohusiana na ugaidi”, kulingana na GTI. Katika taarifa yake siku moja baada ya utekaji nyara huo, wizara ya mambo ya nje ya India iliwataka raia wanaoishi Mali “kuchukua tahadhari kubwa, kuwa macho na kuwa na mawasiliano ya karibu na ubalozi wa India katika [mji mkuu wa Mali] Bamako”.

Wanaume hao walichukuliwa kutoka kwa Kiwanda cha Saruji cha Almasi, kinachoendeshwa na kampuni ya India-biashara ya Prasaditya Group, katika jiji la Kayes. Kampuni na kiwanda hazijatoa taarifa yoyote hadi sasa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment