Mtoto aliyeibiwa apatikana baada ya miaka 48

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

d
Maelezo ya picha,Adriana Metz (kushoto) ametumia miongo kadhaa kumtafuta kaka yake aliyepotea

Mwanaume ambaye alichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa Mama yake akiwa mtoto mchanga wakati wa utawala wa kijeshi wa Argentina na kulelewa na watu asiowajua ametambuliwa baada ya miaka 48, kutokana na kipimo cha DNA.

Dada wa mwanaume huyo, Adriana Metz, ambaye amekuwa akimtafuta kaka yake aliyempoteza kwa miongo kadhaa, alikuwa amezungumza na kaka yake kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.

Metz aliweza kumpata kaka yake kwa usaidizi wa kikundi cha kampeni cha Grandmothers of the Plaza de Mayo, ambacho kwa muda mrefu kinawaunganisha na familia zao watoto wanaokadiriwa kufikia 500 walioibiwa na utawala wa kijeshi.

Kakake Bi Metz, ambaye utambulisho wake haujafichuliwa hadharani, ndiye mtoto wa 140 ambaye kundi hilo limempata.

Katika mkutano na wanahabari, mwanzilishi wa Grandmothers wa Plaza de Mayo, Estela de Carlotto, alisoma taarifa huku wafanyakazi wa kikundi hicho wakipiga makofi na kushangilia.

“Leo tunamkaribisha mtoto wa Graciela Alicia Romero na Raúl Eugenio Metz,” mzee huyo wa miaka 94 alisema, akiwa ameketi karibu na Adriana Metz.

Wazazi wa mwanaume huyo walikuwa ni wanaharakti wa kisiasa, huko Bahía Blanca, katika jiji la Buenos Aires province. Baba yake akiitwa Raúl Metz na mama yake ni Graciela Romero.

Muda mfupi baada ya kunyakua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi mnamo Machi 1976, utawala wa kijeshi ulijaribu kutokomeza upinzani wowote kwa utawala wake kwa kuwakusanya wakosoaji.

Maelfu walitekwa na kuzuiliwa katika vituo vya siri. Wengi waliteswa. Mashirika ya haki za binadamu yanakadiria kuwa takriban watu 30,000 waliuawa au kutoweka kati ya 1976 na mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1983.

Walionusurika waliwaambia Grandmothers of the Plaza de Mayo, kwamba Graciela Romero alijifungua mtoto wa kiume tarehe 17 Aprili 1977 akiwa kifungoni katika kizuizi cha siri kinachojulikana kama “La Escuelita.”

Wafungwa wenzao wanasema kuwa Romero na Metz waliteswa kimwili na kisaikolojia wakiwa kifungoni, kabla ya kutoweka.

Wawili hao wameorodheshwa kama waliotoweka na wanahofiwa kuwa miongoni mwa wanaharakati wengi wa mrengo wa kushoto waliouawa na utawala wa kijeshi.

Binti yao Adriana mwenye umri wa mwaka mmoja alitunzwa kwanza na majirani na kisha walimkabidhi mtoto huyo mchanga kwa babu na bibi yake.

Grandmothers of the Plaza de Mayo wanasema walipewa taarifa juu ya mwanaume huyo na mtu wasiyemjua. Kisha kwa kushirikiana Tume ya Vitambulisho vya Kitaifa (Conadi), chombo rasmi kilichoundwa kutafuta watoto waliotekwa nyara na jeshi, walimwendea mwanaume huyo mnamo Aprili na kumpa kipimo cha DNA.

Alikubali kufanya kipimo, na Ijumaa, Conadi ilimweleza kwamba yeye ndiye mtoto aliyenyakuliwa kutoka kwa Graciela Romero mnamo 1977.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment