Palestine Action yapigwa marufuku baada ya jaji kukataa kuizuia kwa muda

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la Palestine Action limepigwa marufuku baada ya jaji kukataa ombi lake la kuizuia kwa muda serikali ya Uingereza kulitangaza kama kundi la kigaidi.

Siku ya Ijumaa, jaji wa Mahakama Kuu alikataa ombi la kusitisha marufuku hiyo kwa muda.

kundi hilo lilipinga uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa, ambayo Ijumaa jioni ilikataa rufaa hiyo ya dakika za mwisho.

Marufuku hiyo – ambayo ilianza kutekelezwa siku ya Jumamosi – inamaanisha kuunga mkono kundi la Palestina Action itakuwa kosa la jinai, na uanachama au kuelezea kuunga mkono kundi hilo ni kosa lenye adhabu ya hadi miaka 14 jela.

Wakati wa uamuzi wake, alikataa ombi la kundi hilo la kuzuiwa kwa muda, jaji wa Mahakama Kuu Bw Jaji Chamberlain alisema: “Nimehitimisha kwamba athari ambazo zinaweza kutokea ikiwa zuio la muda litakataliwa lakini madai hayo hayana uzito kushinda maslahi makubwa ya umma ya kudumisha amri hiyo.”

Mapema wiki hii, rasimu ya agizo ilifikishwa mbele ya Bunge kuomba marekebisho ya Sheria ya Ugaidi ya 2000 ili kujumuisha shirika la Action Palestina kama lililopigwa marufuku.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment