Usalama waimarishwa kabla ya mazishi ya mwanablogu wa Kenya Albert Ojwang

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Viongozi wakuu wa usalama kutoka makao makuu Kisumu, magharibi mwa Kenya wamewasili Kaunti ya Homa Bay, kabla ya mazishi mwanablogu na mwalimu Albert Ojwang.

Ojwang alifariki mikononi mwa polisi jijini Nairobi mnamo Juni 7 baada ya kukamatwa huko Homa Bay.

Umati wa watu ulivamia na kuteketeza kituo cha polisi cha Mawego wakati mwili wa Ojwang ulifikishwa nyumbani kwao kuagwa na wanakijiji kuelekea mazishi yake hii leo.

Mwili wa Albert uliratibiwa kuagwa katika Shule ya Msingi ya Nyawango, lakini ratiba ilibadilika wakati vijana walipoingilia msafara wa mwanablogu aliyeuawa takriban kilomita moja kutoka nyumbani kwao kijijini katika kijiji cha Kokwanyo.

Vijana walibeba jeneza la Albert na kuupeleka katika Kituo cha Polisi cha Mawego, ambako mmoja wao aliyekuwa akiongoza msafara huo alikamatwa na kuwekwa kizuizini.

Vijana hao inadaiwa kuwa waliiba nguzo za bendera ya polisi na bendera za taifa, pamoja na nembo za kituo, walipokuwa wakitoroka eneo la tukio baada ya polisi kuwarushia bomu la machozi kuwatawanya.

Polisi wanaoishi karibu na hapo walisema nyumba zao ziliporwa. Hakuna mtu aliyejeruhiwa kujeruhiwa katika rabsha hizo, polisi walisema.

Uchunguzi umeanzishwa kuwabaini waliopanga na kutekeleza tukio hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment