Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa makampuni kadhaa ya kimataifa kuacha kufanya biashara na Israel, akionya kwamba yanaweza kuhusika katika uhalifu wa kivita huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Akiwasilisha ripoti yake kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Francesca Albanese, alielezea kile alichokiita “uchumi wa mauaji ya halaiki” na kusema kuwa vita vinavyoendelea dhidi ya Hamas vimeipa Israel fursa ya kufanya majaribio ya silaha na teknolojia mpya bila uwajibikaji au uangalizi.
Israel haijaafiki ripoti hiyo, ikiiita “isiyo na msingi” na kusema kwamba “ripoti hii itaongezwa kwenye jalala la historia.”
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa au wanahabari maalum, ingawa wameteuliwa na shirika, wako huru.
Bi. Albanese ni wakili wa kimataifa kutoka Italia, anayejulikana kwa kauli zake za wazi na kali. Hapo awali aliripoti kwamba Israel inafanya mauaji ya halaiki huko Gaza.
Alirudia mashtaka hayo siku ya Alhamisi, akisema Israel ilikuwa ikifanya “moja ya mauaji ya kikatili zaidi katika historia ya kisasa.”
Katika ripoti yake mpya, Albanese aliyataja makampuni ambayo, kulingana na yeye, yananufaika kutokana na uhalifu wa kivita katika vita vya Gaza na hivyo kuwachukulia kama washirika.
Orodha hiyo inajumuisha kampuni ya silaha ya Marekani ya Lockheed Martin, ambayo imeiuzia Israel silaha, na makampuni ya teknolojia kama vile Alphabet, kampuni mama ya Google, IBM, Microsoft na Amazon, ambayo anasema imeipatia Israel teknolojia ambayo inaitumia kufuatilia na kuwalenga Wapalestina.
Caterpillar, Hyundai, na Volvo pia wametajwa, huku ripoti ikidai kuwa kampuni hizi zinasambaza magari yanayotumika kubomoa nyumba na kusafisha maeneo yaliyopigwa na mabomu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.