Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makakama kuu ya Gujarat nchini India imeanza kusikiliza kesi dhidi ya wakili ambaye alionekana kwenye video akinywa bia na na kuzugumza kwenye simu yake wakati akihudhuria kesi ya kawaida.
Picha ya video ya Wakili wa Mahakama Kuu ya Gujarat, Bhaskar Tanna akidaiwa kunywa bia ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Video hii hiyo iligeuka kuwa kitovu cha mjadala punde tu iliposambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mahakama Kuu ya Gujarat imeamuru kuchukua hatua ya kali dhidi ya Bhaskar Tanna kwa ‘dharau’.
Mahakama Kuu ya Gujarat mnamo Jumanne, Julai 1, iliita tabia yake ‘ya matusi na ya kusikitisha’.
Kulingana na shirika la habari la PTI, Mahakama Kuu ilikuwa imemchukulia hatua ya nidhamu kwa tabia hii na kumshitaki kwa kukosa maadili.
Mahakama Kuu imemtaka Msajili wa mahakama kutoa onyo kwa Bhaskar Tanna na imepiga marufuku kuonekana kwake kwenye kesi hiyo aliyokuwa akiiendesha.

Akijitetea kuhusu tukio hilo Wakili Bhaskar Tanna alisema , “Video hii ya sekunde 15 nilionyeshwa mahakamani. Nimeomba msamaha bila masharti kwa majaji wote wawili mara mbili katika suala hili.”
Alifafanua zaidi kwamba , “Hii ilitokea nilipobonyeza kitufe cha video kwa bahati mbaya badala ya sauti. Hata hivyo, niliizima mara moja ndani ya dakika chache. Lakini haikutokea wakati wa usikilizwaji wa kesi unaoendelea, usikilizwaji ulikuwa umekwisha.”
Kwa mujibu wa sheria ya kudharau mahakama ya mwaka 1971, nchini India, katika tukio kama hili , Wakili anaweza kuadhibiwa kwa kifungo kisichozidi miezi sita jela au faini au vyote kwa pamoja.
Kesi hiyo imeahirishwa sasa, itasikilizwa baada ya wiki mbili.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.