Njia Nne Za Kutambua Kiwango Cha Mtaji Ambacho Unahitaji…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Gharama Za Awali Za Kuanza Biashara.

ii. Gharama Za Uendeshaji Wa Biashara.

iii. Fuatilia/Jifunze Kwa Wanaofanya Tayari.

iv. Uwe Na Bajeti Iliyoandikwa

Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia Ya Pili

– Gharama Za Uendeshaji Wa Biashara.

Wapo wengi wanafanikiwa kuanzisha biashara ila hawadumu kwenye hizo biashara.

Sababu mojawapo ni kuwa wanakuja kugundua kuwa, gharama ya uendeshaji ni kubwa kuliko hata ya kuanzisha biashara yenyewe.

Kumbuka kuwa, kuna baadhi ya biashara ambazo itachukua muda kuanza kupata faida, hivyo ni lazima uendelee kuifanya kwa muda fulani kabla haijaanza kukuzalishia faida.

Kwenye aina hii ya biashara ni lazima uwe na uwezo wa kuiendesha kwa muda fulani kabla haujapata faida.

Mtaji wa uendeshaji (Operational Capital) unahusisha zile gharama unazohitaji ili biashara yako iendelee.

Hapa inaweza kuwa ni pamoja na mishahara ya kuendelea kulipa wafanyakazi, kulipia umeme na maji, kodi za halmashauri n.k.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment