Mahitaji Matano Utakayotaka Kuhudumia…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. The Drive to Bond (Kuunganika na Watu)

ii. The Drive to Acquire (Kupata na Kumiliki)

iii.The Drive to Learn (Kujifunza

iv. The Drive to Defend (Kujilinda

v. The Drive to Feel (Kuridhisha Hisia)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Hitaji La Tano

– The Drive to Feel (Kuridhisha Hisia)

Hitaji la kupata hisia nzuri ni moja ya eneo muhimu na kubwa sana ambalo unaweza kulifanyia kazi unapotaka kuanzisha biashara yako.

Kila mwanadamu wa kawaida, mara tu anapoamka huwa anatamani sana kuanza kujisikia vizuri.

Kama utaweza kufanya biashara yoyote ile ambayo inalenga kumsaidia mtu ajisikie vizuri katika hisia zake basi utakuwa umegusa eneo la muhimu sana la hitaji la mtu.

Ni ukweli usiopingika kuwa, hili ni eneo mojawapo ambalo mtu akiguswa vizuri basi anakuwa tayari kutumia pesa nyingi sana na mara nyingi nguvu ya hisia huwa ni kubwa sana kuliko akili inapofika kwenye suala la mtu kutumia pesa yake.

Hii ndio maana “Entertainment Industry” ni moja ya eneo ambalo lina pesa nyingi sana duniani.

Hii inajumuisha vitu kama muziki, mpira wa miguu, matamasha mbalimbali n.k

Kumbuka kama tutakavyoona kwenye vigezo vya kuchagua biashara, sio lazima ufanye kile ambacho kinaangukia hapa, unaweza kuwa sehemu ya watoa huduma wa eneo hilo.

Kwenye kila biashara kuna mnyororo mkubwa ambao wewe unatakiwa kuchagua eneo ambalo unataka kujichomeka ili uweze kufanya biashara.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment