Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hatua ya Donald Trump kupunguza kiwango kikubwa cha ufadhili wa Marekani kuelekea misaada ya kibinadamu ya kigeni inaweza kusababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 14 ifikapo mwaka 2030, kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu la The Lancet.
Theluthi moja ya wale walio katika hatari ya kukabiliwa na vifo vya mapema ni watoto, utafiti umebaini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema mwezi Machi kwamba utawala wa Rais Trump ulifuta zaidi ya asilimia 80 ya programu zote katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, USAID.
“Kwa nchi nyingi za kipato cha chini na wastani, mshtuko unaosababishwa unaweza kulinganishwa kwa kiwango na janga la kimataifa au mzozo mkubwa wa silaha,” Davide Rasella, ambaye aliandika ripoti ya Lancet, alisema katika taarifa.
Kusishwa ghafla kwa ufadhili huo “kunatishia kurudisha nyuma”- hatua zilizopigwa miongo miwili iliyopota katika juhudi za kuimarisha afya miongoni mwa watu walio katika hatari,” aliongeza Rasella, mtafiti katika Taasisi ya Barcelona ya Afya Ulimwenguni.
Ripoti hiyo inakuja wakati makumi ya viongozi wa dunia wanakutana katika mji wa Seville nchini Uhispania wiki hii kwa mkutano wa misaada unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.
Watafiti hao wa walichambua data kutoka mataifa 133, kukadiria kuwa ufadhili wa USAID ulikuwa umezuia vifo milioni 91 katika nchi zinazoendelea kati ya 2001 na 2021.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.