Aina 5 Za Wagahirishaji…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. WapendaMzuka (Thrill Seeker)

ii. Wanaoendeshwa na Maoni ya Watu

iii. Wanaoogopa Kulipia Gharama ya Maamuzi Yao

iv. Wanaosubiri Ukamilifu wa Jambo

v. Wanaojirundikia Mambo Mengi Pasipokuwa na Umuhimu (Busy Procrastinators)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Tatu

– Wanaojirundikia Mambo Mengi Pasipokuwa na Umuhimu (Busy Procrastinators)

Hivi umeshawahi kukutana na mtu ambaye yuko bize sana…

…ila hakuna matokeo makubwa kwenye maisha yake?

Kuna watu kila ukikutana nao wanaonekana wana mambo mengi sana…

…na wako bize sana na maisha yao ila maisha huwa hayaendani na ubize wao.

Je, wewe ni mmoja wao?

Watu wa namna hii ukweli ni kuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa…

…kughairisha ambao unaangukia katika kundi hili.

Ni watu ambao kila wakati wako bize.

Ila tatizo lao ni kuwa wanakuwa bize na mambo ambayo…

…sio ya muhimu kwenye maisha yao.

Na wanaacha kufanya na kuzingatia mambo ambayo ni ya muhimu zaidi.

Kinachofanya watu wafanikiwe sio kwa sababu wako bize sana…

…kufanya mambo mengi kwenye maisha yao.

Bali ni kwa sababu wanafanya mambo sahihi kwenye maisha yao.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment