Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Wanafanya wanachokipenda, wana ujuzi nacho ila hakiwaingizii pesa kwa sasa.
ii. Wanachofanya kinawalipa vizuri, wana ujuzi nacho ila hawakipendi.
iii. Wanapenda kufanya wanachofanya, inawalipa, ila ujuzi ni mdogo na kama wakiongeza ujuzi basi watalipwa Zaidi.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Kundi La Kwanza
– Wanafanya wanachokipenda, wana ujuzi nacho ila hakiwaingizii pesa kwa sasa.
Kundi hili lina watu ambao tayari wanajua passion yao na wameshafanya maamuzi ya kuishi kwenye passion zao tayari.
Mara nyingi watu walio katika kundi hili huwa ni wavumilivu sana na wanaamini kuna siku mambo yatabadilika na wataanza kuona matunda ya bidii yao.
Hawa ndio watu wanaoongoza kwa kutoeleweka na watu wao wa karibu na jamii kwa ujumla.
Watu walio katika kundi hili, huwa wanaweza kuacha kazi nzuri au wakaacha kufanya kitu kinachoendana na taaluma yao na wakaenda kufanya kitu tofauti kabisa.
Mara nyingi watu wengi huwaona wamechanganyikiwa kwa sababu huwa wanaongoza kwa kuona vitu ambavyo wengine hawavioni.
Kama utajikuta kwenye kundi hili na ukaona kabisa unachofanya unakipenda sana, na una ujuzi nao wa kutosha bila shaka kabisa ila hakikulipi.
Kuna mambo muhimu unatakiwa uyawekee mkazo.
Cha kwanza ni kuhakikisha unaongeza ujuzi wako wa kibiashara (Business Skills) hasa katika eneo la masoko na mauzo (Marketing and Sales).
Watu wengi sana walioko kwenye kundi hili, huwa wanakuwa na uwezo mzuri, mawazo mazuri na mipango mizuri, wanachopungukiwa na uwezo wao wa kibiashara wa kubadilisha walichonacho kukifanya kuwa pesa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.