Tabia Tatu Za Watu Wanaofanikiwa…….

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Uwezo wake wa kuwa na ujuzi wa kitaalamu katika kile anachokifanya (Technical skills).

ii. Eneo la pili liliitwa “Human Engineering” kwa sasa hujulikana zaidi kama “Emotional Inteligence (EI).

iii. Kutambua hisia za wengine na kuhusiana nao kwa uangalifu.

Katika Makala Hii Tutazungumzia Eneo la pili

– “Human Engineering” kwa sasa hujulikana zaidi kama “Emotional Inteligence” (EI).

Eneo hili huchangia asilimia 85 ya mafanikio yako.

Watu wengi kwa kutokujua umuhimu wa eneo hili wameshindwa kujifunza na kuwekeza, matokeo yake wanajikuta wana ujuzi mkubwa wa kufanya kazi zao lakini wanafeli kufanikiwa katika eneo hili.

Eneo hili linahusiana na uwezo wako wa kuthibiti hisia zako na kutoruhusu kupelekeshwa na matukio ambayo yametokea na yanataka kukuharibia mwelekeo wako wa maisha.

Mara nyingi fursa kubwa zinapokaribia katika maisha yetu tunajikuta kuna mambo ambayo yanatokea na usipokuwa mwangalifu utajikuta yanakupotezea kabisa mwelekeo wa siku yako.

Umeshawahi kuamka siku na unakusudia kufanya jambo fulani la muhimu na ghafla mtu anasema neno fulani au kukufanyia kitu fulani ambacho kinakuharibia kabisa siku yako?

Kama ikikutokea hivi maana yake ni 49kuwa uwezo wako wa Human Engineering bado ni mdogosana.

Kuna watu wanashindwa kabisa kuendelea mbele kwenye maisha yao kwa sababu ya mambo ambayo yamewatokea na yamewaumiza mioyo yao.

Eneo lingine la Human Engineering ni kutambua hisia za wengine na kuhusiana nao kwa uangalifu.

Kila siku kuna watu utakutana nao ambao wamekata tamaa na wanataka na wewe ukate tamaa kuhusu ndoto ulizonazo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment