Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wachunguzi wamepata data ya vifaa vya kunasa mwenendo wa ndege ya shirika la Air India iliyoanguka mapema mwezi huu, wizara ya usafiri wa anga imethibitisha, kuashiria hatua muhimu katika uchunguzi huo.
Takriban watu 270 walifariki wakati ndege ya Boeing 787-8 iliyokuwa ikielekea London ilipoanguka dakika moja baada ya kuanza safari Juni 12 kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad magharibi mwa India.
Wachunguzi hapo awali walikuwa wamepata vifaa vyote viwili vya kunakili mwenendo wa Ndege vilivyoboreshwa (EAFs) – “Black Box” – kutoka eneo la ajali ya Boeing 787 tarehe 13 na 16 Juni – moja kutoka juu ya paa, nyingine kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya serikali ya India kutoa maelezo yaliyokusanywa kutoka kvifaa hivyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.