Aina 8 Za ‘’CORE GENIUS”…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Verbal-Linguistic Intelligence ( Word Smart)
ii. Logical – Mathematical Intelligence (Number Smart)
iii. Spatial Intelligence – Picture Smart
iv. Bodily – Kinesthetic Intelligence (Body Smart)
v. Musical intelligence (music smart)
vi. Naturalist intelligence (Nature Smart)
vii. Intraperson intelligence (self-smart)
viii. Interperson intelligence ( People smart)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Tatu

– Spatial Intelligence – Picture Smart

Hawa ni watu ambao, sehemu yao ya ubongo inayohusiana na picha na matukio ina nguvu zaidi kuliko eneo lingine lolote la ubongo wao.

Utawajuaje watu hawa?

Wanakumbuka matukio mbalimbali kwa kuona zaidi kuliko kusoma Wanakumbuka rangi mbalimbali za nguo za watu, majengo, magari, n.k

Wanaweza kueleze vizuri hadi anayesikiliza akajenga picha ya wanachoongea Wanapenda kuchora picha mbalimbali hata kama sio wachoraji wazuri sana Wanapenda kumechisha rangi mfano, mavazi, nyumbani, simu, n.k

Wanapenda sana kuona picha, na wanapenda filamu (movies).

Mfano wakienda kwenye harusi, wanaelezea kwa picha bi harusi alipendeza sana, wataeleza kuhusiana na shela, viatu, msimamizi wake n.k

kisha wataelezea kuhusu ukumbi ulivyopambwa na wageni walivyotokelezea vizuri n.k

Akianza kukuelekeza mahali anataja kila kitu ambacho kitakusaidia kufika unapokwenda.

Atataja majengo na rangi zake, mitindo ya nyumba, aina za maduka n.k

Wana kumbukumbu sana na maeneo mbalimbali na hawapotei kirahisi hata kama walifika mara moja.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment